Home Blog

Kichekesho cha Bwana Harusi Kikojozi

1

Jamaa alikuwa ana tabia ya kukojoa kitandani baadhi ya siku.
Akafikia kuoa. Katika ya siku za mwanzo baada ya harusi, siku moja kama kawaida yake alijikojolea.
Akapiga kelele “Mungu wangu eee”.
Mke wake akashtuka, akamuuliza: Vipi mume wangu?
Mume: Hivi mke wangu ungeota unataka kuliwa na mamba, chuwi na simba kwa wakati mmoja ungefanyaje?
Mke: Ningezimia kabisa.
Mume: Basi mwenzio sijazimia nimejikojolea.

 

Vichekesho vya Kesi ya Mmasai na Mpare

0
Masai na ngombe

Kulikuwa na wizi ulifanyika katika nyumba moja ya mpare pale hedaru na muhusika baada ya kufuatilia aligundua kuwa aliyemuibia ng’ombe wake alikuwa ni mmasai mmoja wa ng’ambo ya pili ya mto kikuletwa.

Mpare alimfungulia kesi ya wizi mmasai na mahojiano mahakamani yalikuwa kama ifuatavyo:

Mmasai; Wewe anasema mimi ameiba hiyo ng’ombe yako?

Mpare; Ndiyo

Mmasai; Aliingia kwa mlango ya nyuma ama ya mbele?

Mpare; Ya nyuma

Mmasai; Mekosa, aliingia kwa mlango ya mbele ya nyumba

Mmasai; Je, aliswaga ng’ombe dume akatangulia mbele au alikuwa nyuma?

Mpare; Dume alitangulia mbele

Mmasai; Mekosa tena, alibaki nyuma

Mmasai; Je ng’ombe alioibiwa iko ngapi?

Mpare; Ng’ombe  7

Mmasai; Amekosa kabisa, ng’ombe alikuwa 5 tu!!

Aha ha ha

Wewe hisi jaji alimhukumu au alimuachia huru huyo mmasai?

 

 

Chapati Thief Kansiime Anne – African Comedy

0

What!!? U have not Subscribed yet??? Eh nga you are a RISK -TAKER!!
NOW NEW CLIPS EVERY TUESDAY AND FRIDAY!!!
pls also like me on facebook
https://www.facebook.com/pages/Kansiime-Anne-Entertainer/263758240421584?ref=ts&fref=ts

Sleepy drunkard. Kansiime Anne. – African Comedy.

0

What!!? U have not Subscribed yet??? Eh nga you are a RISK -TAKER!!
NOW NEW CLIPS EVERY WEEK!!!
pls also

Vickekesho na Vituko vya Uzamiaji wa Kwenye Misiba

0
Kituko cha uzamiaji wa kwenye misiba

Kituko cha uzamiaji wa kwenye misibaHapa duniani vituko haviachi kwisha, jamaa mmoja alitoa kichekesho cha mwaka katika moja ya uzamiaji wake wa kwenye misiba kutoka Arusha, siku moja katika pitapita yake aliingia mtaa mmoja na katika kutembea kidogo akakutana na nyumba yenye msiba.

Jamaa kama kawaida yake akazamia na kwa bahati nzuri akakuta ndo waombolezaji waliokuwa wamekesha hapo walikuwa wanapata uji wa moto ili kufukuza baridi. Jamaa naye yumo akapata kikombe chake na kwa bahati mbaya akapaliwa na uji wa moto kiasi cha kutokwa na machozi. Wale wenzake msibani wakaanza kumpa pole.

Ili kupotezea kwamba hajaunguzwa na uji akaanza kusema (huku akionekana analia kwa sababu ya yale machozi)

“MAREHEMU ALIKUWA MTU MZURI SANA” “YAANI ALIKUWA ANAPENDA WATU” “TAIFA LIMEPOTEZA TUNU MUHIMU SANA” “MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI”.

Kumbe aliyekuwa anazikwa ni katoto ka siku moja tu! Wazamiaji bwana!!

Kichekesho cha Urais na Jela

0

Kwame Nkrumah alitoka jela akawa rais.

Nelson Mandela nae alitoka jela akawa rais.

Pia Obasanjo. Theodore Orji alitoka jela akawa gavana. Omisore Iyiola alitoka jela akawa seneta.

Al Mustapha alitoka jela akawa brigedia.

Robert Mugabe alitoka jela akawa waziri mkuu, na baadae rais na mpaka sasa ni rais.

Ndugu yangu amini usiamini, rais wetu mwaka 2015 ni BABU SEA