Akaunti za Email Milioni 500 za Yahoo Zatekwa Nyara

0
357
Email za Yahoo zatekwa Nyara

Hello wanajukwaa japo ilitokea mwaka 2014 mwishoni lakini kuna mambo ya kukumbushana kuhusu email zetu.

Yahoo imehackiwa/ilitekwa nyara mwishoni mwa mwaka juzi na Uongozi wa Yahoo wamekiri kutokea hilo. Yahoo wanawashauri wateja wao kubadili neno la siri. Jumla ya barua pepe milioni 500 ziliibwa na watekaji na hakuna ajuaye wanategemea kuyafanyia nini hizo emails

Maelezo zaidi.  http://money.cnn.com/2016/09/22/technology/yahoo-data-breach/

Maelezo muhimu juu ya usalama wa email yako soma zaidi hapa chini

  1. Usihifadhi taarifa nyeti kama credit card na passwords muhimu kwenye email
  2. Tumia password ndefu na yenye herufi mchanyako angalau herufi kubwa na ndogo, number na zile special character. Kama ukitumia maneno yanayoeleweka usitumie majina y akiingereza, au ya lugha yeyote maarufu, usitumie lugha ya kingereza kabisa. Tumia maneno ya ndani ya lugha yako ukiunganisha na number na special character mfano Nndizi12&nyama
  3. Badilisha neno la siri angalau kila mwaka au miezi sita
  4. Kama utatumia Maswali, tumia maswali ambayo majibu yake ni siri yako. Taja Jina la baba yako. Hili swali jibu lake linaweza kujulikana. Taja jina la mwalimu wako wa shule ya msingi. Jibu la hili swali ni ngumu kutabiri na ndilo swali zuri
  5. Ukihisi mwenendo wa kukutia wasiwasi kwenye email yako badilisha neno la siri kwa haraka
  6. Usiandike neno la siri popote au kama ukiandika usiandike peke yake. Mfano uanweza kuandika kwenye diary hii password Nndizi12&nyama hivi Tangu utotoni nilipenda kula Nndizi 12 na nyama
  7. Unapoingia kwenye email kwa kutumia computer ambayo sio ya kwako hakikisha unaondoa tick kwenye kisanduku cha remember me. Pia browser inapokutaka kukumbuka password yako chagua hapana milele “do not remeber password forever”
  8. Ukipoteza au kumisplace simu yako sehemu usiyojua ingia kwenye email badilisha password na ukiweza futa email zilizoko kwenye simu yako iliyopotea

Taarifa Zinazofanana

Save

Leave your comment about Akaunti za Email Milioni 500 za Yahoo Zatekwa Nyara using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here