Baada ya wenzao wa Acacia Mining kuishitaki serijali ya Tanzania wiki iliyopita, kampuni ya tatu kwa ukubwa ya uchimbaji wa dhahabu duniani imetangaza kuanza mchakato wa kuishitaki Tanzania kwenye mahakama ya UN baada ya kupitisha sheria mpya ya madini inayoruhusu mikataba ya zamani kupitiwa upya. Wamesema wanafanya hivyo kwa usalama wao kwani wanadai masharti ya mkataba wa zamani ndio uliowashawishi kufanya maamuzi ya kufanya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania yapata takribani miaka 20 iliyopita.
AngloGold ni kampuni yenye makao makuu Afrika ya Kusini na ndio wanaomiliki mgodi wa Geita Gold Mine na migodi mingine mingi duniani.
Wiki iliyopita Kampuni ya Acacia inayomiliki migodi ya Buzwagi, Bulyaghulu na North Mara nao wamefungua jaladala kesi kama kinga juu ya mkata wao wa zamani usiingiliwe na sheria mpya ya madini.
http://www.mining.com/anglogold-taking-tanzania-un-court-countrys-new-mining-law/