Askofu Gwajima Atiwa Mbaroni kwa Kumtukana Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo

0
1193

 Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima atakiwa kufika haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za  kumkashfu na kumtukana Askofu Polycarp Pengo
 Askofu Gwajima
“Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na Youtube na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine”.
 Kadinali Polycarp Pengo
Baada yajeshi la polisi kumtafuta Askofu Gwajima na kumkosa wamemtaka aripoti kituoni mwenyewe kwa haraka bila kukosa
Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.
Askofu Gwajima anashutumiwa kumtukana Kardinali Pengo kuwa yeye ni mjinga, mpuuzi, hana akili, asiyefaa, kazeeka, kuna mtu anampigia debe, kawaibisha maaskofu wenzake na wakristo wote Tanzania, kama mtoto mdogo aliyevaa pampers, mlevi, na ukome

Leave your comment about Askofu Gwajima Atiwa Mbaroni kwa Kumtukana Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo using the comment form below