Edward Lowassa Kuihama CHADEMA

0
475

Wazili Mkuu ALIYEJIUZULU kwa kashfa, Edward Lowasa ambaye mwaka jana alijiengua kutoka CCM na kuhamia CHADEMA, anatajariwa kukihama nacho na kuingia chama kingine wakati wowote kuanzia sasa.

Tayari Lowasa amemtanguliza mmoja kati ya “maswahiba” wake wakubwa wa kisiasa, Goodluck Ole Medeye (UDP) ili kuandaa “Mapito ya Bwana” kama ilivyokuwa kwa Yohana Mbatizaji, yule ambaye alifanya hivyo kwa ajili ya Yesu wa Nazareth kwa mujibu wa Vitabu vitakatifu.

Mwaka uliopita, Medeye naye alijiengua CCM akikerwa na hatua ya Kamati kuu ya Chama hicho kuliengua jina la Lowasa katika kinyang’anyiro cha uteuzi wa mgombea wa kiti cha uraisi, lakini alianza kwa kukanusha kujiunga rasmi chadema kwa kusema ni mshauri wa kisiasa wa mbunge huyo wa zamani wa Monduli, mkoa wa Arusha.

Lakini wmezi uliopita, Medeye aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, alijiengua tena Chadema na kuhamia UDP na kuteuliwa na Kamati Kuu ya Chama hicho, siku hiyohiyo kuwa Kaimu Katibu Mkuu.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya chama hicho zinasema kuwa hatua ya mwanasiasa huyo kuhamia huko haikuja kama bahati mbaya, nali kilichofanyika ni kutangulizwa na Lowasa kabla yeye mwenyewe hajafanya hivyo pia hapo baadaye.

Inagwa haikuthibitishwa mara moja kutokana na kutopatikana kwa Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, habari zilizolifikia gazeti hili saa chache kabla ya kuingia mitamboni jana, zinasema wanasiasa hao wawili tayari wamefikia makubaliano ya kukabidhiana madaraka kwa mbunge huyo wa zamani wa Bariadi Mashariki mkoani Simiyu, kustaafu kukiongoza chama hicho.

Chanzo cha habari hizi kinasema baada ya kuzidiwa takribani kura 2,200,000 tu hivi na Raisi John Magufuli katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015, wataalamu na washauri wa kisiasa wa Lowasa aliyegombea pia wadhifa huo kupitia Chadema, walifanya utafiti na kugundua kwamba angeshinda kama angefanya vizuri katika mikoa iliyopo kanda ya Ziwa.

“Utafiti wao unaonyesha kwamba ushindi wa Magufuli ulikuwa mkubwa Zaidi katika eneo hilo, ;akini alifanya vibaya sanna katika Kanda za Kaskazini hususan ya Arusha na Kilimanjaro ambako Lowasa alishinda kwa Zaidi ya 80%, kimesema chanzo hicho cha habari ambacho hata hivyo hakikutaka kutaja jina lake.

Msukumo mkubwa wa Lowasa kuanza kujipanga kuihama Chadema umeelezwa kuwa kutokana na kugonga ukuta kwa nia yake ya kutaka kugombea uenyekiti wa chama hicho, nafasi ambayo sasa inashikiliwa na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ambaye naye hataki kuiachia.

Mbowe aliyeshika wadhifa huo mwaka 2004, akiurithi kutoka kwa mtangulizi wake, Bob Makani ambaye kwa sasa ni marehemu, amekuwa akigombea peke yake tokea wakati huo na mwaka 2009, kiongozi huyo aliingia kwenye mgogoro mkubwa baina yake na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Zitto Kabwe ambaye alijitosa kutaka kumng’oa.

Pamoja na kuwepo na baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho waliotaka naye astaafu kama walivyofanya watangulizi wake, Mzee Edwin Mtei na baadaye Marehemu Bob makani ili wadhifa huo sasa ushikwe na mtu mwingine, Mbowe na wapambe wake katika upande wao nao wameelezwa kwamba hawapo tayari kuona jambo hilo linatokea.

Hali hiyo ndiyo imemlazimisha Lowasa na wafuasi wake kuamua kuondoka na kufuata chama kingine ambapo, hapo ndipo ikapatikana UDP kutokana kwa sababu kubwa mbili.

Kwanza, Cheyo ambaye amekuwepo madarakani akiwa Mwenyekiti wa chama hicho tokea kianzishwe takribani miaka 25 iliyopita, inaelezwa kuwa ‘amechoka’ kisiasa na kifedha, hivyo alichokuwa anatafuta ni kupokelewa nafasi hiyo na mtu mwingine, lakini alikuwa hajapatikana kutoka ndani ya chama hicho chenyewe, fursa iliyoonekana kuwa nzuri kwa Lowasa kwenda kumrithi kwa kuhamia huko.

Sababu ya pili iliyoelezwa na kundi la Lowasa kutafuta chama cha siasa ambacho itakuwa rahisi kwao kupokelewa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hivyo ikaonekana kuwa UDP ndilo eneo muafaka kwa vile inasemakana kwamba inafahamika vya kutosha katika eneo hilo.

Mikoa iliyolengwa Zaidi ili kufikia lengo la kupata kura nyingi kwa Lowasa na kushinda kiti cha Uraisi katika uchaguzi mkuu ujao 2020 ni Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Geita, Tabora na Singida ambayo mwaka jana inaaminika kwamba ‘ilimbeba’ Raisi Magufuli kuipata nafasi hiyo.

“Kwa hiyo, Medeye ametangulizwa na haya ni makubaliano kati ya Lowasa na Cheyo mwenyewe. Ndiyo maana siku alipopewa kadi ya uanachama ndiyo ileile ambayo pia aliteuliwa kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UDP” kimesema chanzo hicho cha habari.

Kimebainisha kuwa kuhamia kwa Lowasa katika chama hicho, kutaambatana na kundi la baadhi ya waliokuwa wakuu wa wilaya ambao wiki iliyopita ‘walitemwa’ katika uteuzi wa kwanza wa nafasi hizo unaofanywa na Rais Magufuli tangu alipoingia madarakani.

Madai yaliyopo ni kuwa baadhi ya wakuu wa wilaya walioachwa katika uteuzi mpya, wameadhibiwa kwa kutuhumiwa kuendelea kuwa wafuasi wa Lowasa hata baada ya kujiengua kwake kutoka CCM, kisha kuhamia Chadema alikoteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho huku akiungwa mkono na kile kinachoitwa Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA)

Habari hizo zinadai kuwa kwa kutumia nyazifa zao hizo za kisiasa katika uongozi wa serikali, baadhi ya wakuu wa wilaya walikuwa wakiihujumu CCM ili ing;olewe madarakani, na pia walikuwa wakifanya hivyo ili kumsaidia Lowasa ashinde na kuwa Rais wa Serikali ya Awamu yaTano.

Mbali na hao, baadhi ya wabunge wa sasa wa CCM waliokuwa wafuasi wake tangu akiwa katika chama hicho, watajiuzulu nyazifa zao hizo na kuhamia UDP kwenda kuijenga ili iwe imara, lengo likiwa ni kushinda uchaguzi ujao wa mwaka 2020 na kumwingiza ikulu

Pamoja na baadhi yao kutajwa kwa majina na majimbo wanayoyawakilisha bungeni, gazeti hili halikutaka kuyaweka hadharani ingawa wapo wanaofahamika kwa sababu walikuwa pamoja naye ‘kwa muda wote’ kipindi ambacho ilikuwa kabla na wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea wa uraisi kupitia chama hicho kilichopo madarakani.

Mbali na hao, baadhi ya wabunge wa Chadema pia watahama naye kwa kile kinachoelezwa kwamba, Lowasa alitoa fedha nyingi kuoitia kwa viongozi wao wakuu wa chama ili wapewe ziwasaidie kushinda nafasi hizo, lakini hakuna aliyepewa na ikabidi watumie zao weneywe huku wengine wakikopa na kuingia kwenye madeni makubwa

NA MWANDISHI WETU DAR,
MWANAHABARI 5-11 JUL 2016

Leave your comment about Edward Lowassa Kuihama CHADEMA using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here