HATI YA MUUNGANO FEKI AU HALISI?

0
455
HATI YA MUUNGANO FEKI AU HALISI
HATI YA MUUNGANO FEKI AU HALISI

Hatimaye Serikali imeonyesha kwa wananchi HATI YA MUUNGANO. Katika taarifa yake Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue na waandishi wa habari jioni hii mjini Dar es salaam ameonyesha hati ya muungano iliyosainiwa na waasisi wa muungano huo hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume.

Hata hivyo hati hiyo inakosa vitu muhimu vitakavyoihalalisha kuwa hati halisi ya Muungano. Vitu hivyo ni kama Mhuri au kusema moja kwa moja mhuri wa moto ambao ndio rahisi kutofautisha na Hati feki. Angalau basi ungekuwa na mhuri wa opande zote mbili.

Hati hiyo pia imechukua muda kuonyeshwa kwa hiyo kujenga mazingira kwa Watanzania kwamba hati hiyo ilikuwa inaandaliwa kwa kugushiwa na hivyo kutoamini kama ni halisi au feki.

Maoni ya Mh. Tundu Lisu

Hata baada ya Hati ya Muungano kutolewa kwa wajumbe wa Buge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Tundu Lissu, ameendelea kusimamia msimamo wake kuwa hati haipo na iliyoletwa ni feki.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Bunge, Lissu ambaye ndie muibua hoja hiyo alisema; “Hivi hawa wanamghiribu nani? Nasema hiyo hati haikuwahi hata kupelekwa Umoja wa Mataifa.”

Alidai sahihi zilizopo ni feki kwani zinatofautiana na zile zilizopo kwenye hati ya Mabadiliko ya Kwanza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Juni 1965, na zile zilizopo kwenye Hati ya Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha za kigeni na Sheria ya kugawa ardhi kwa Wazanzibari ambazo zote zinafanana.

Lissu alisema kwa miaka 50 haikuwahi kuonyeshwa kwa wabunge sembuse wananchi, haipo Umoja wa Mataifa pamoja na kudaiwa ipelekwe na wala Wanzanzibari hawana. Aliendelea kusema kuwa alimshuhudia Benard Membe (Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) akisema iko UN, jambo ni uwongo mtupu.

Alisema nyaraka kama hizo, zinatakiwa kuwekwa Makumbusho ya Taifa kwa kuwa ni nyaraka wazi zinazotakiwa kuona na kila anayetaka, kwa rahisi.

Aliendelea kutoa mifano kwa kusema kuwa

“Marekani ilipata uhuru zaidi ya miaka 200 iliyopita, lakini kila nyaraka za uhuru zinaonekana kwa rahisi siyo kama huku kwetu ambako mambo yanafanywa kisirisiri  utadhani biashara haramu,”.

Angalia hati yenyewe kwenye picha ambatanishwa halafu utoe maoni yako

Leave your comment about HATI YA MUUNGANO FEKI AU HALISI? using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here