Hotuba ya Dr Slaa Serena Hotel 1 Septemba 2015

0
624
Dr Wilbroad Slaa Akihutubia Serena Hotel Kuachana na Sisa za Vyama 1 Septemba 2015

Date: Tuesday, September 1, 2015

HOTUBA YA DR SLAA SERENA HOTEL 1 SEPTEMBA 2015 KWA UFUPI

 1. Napenda  kumshukuru  mwenyezi mungu  kwa  kutujali  uzima.
 2. Nimeamua  kujitokeza  leo  hii ili  kukomesha  upotoshaji  na  kuuweka  wazi ukweli.
 3. Sina tabia  ya  kuyumbishwa  na  ninasimamia ninachokiamini.
 4. Sina  ugomvi  na  kiongozi  yeyote  maana  siasa  sio uadui.
 5. Siasa  inapoongozwa  kwa  misingi  ya  upotoshaji, matokeo  yake  ni  vurugu.
 6. Naweka  wazi  kuwa  mimi  sikuwa  likizo  na  hakuna  aliyenipa  likizo  yoyote.
 7. Kilichotokea  ni  kuwa  niliamua  kuachana na  siasa  tangu  28.7.2015  saa  sita  usiku  baada  ya  kutoridhishwa  na  kilichokuwa  kinaendelea  ndani  ya  chama changu.
 8. Ni  kweli  nilishiriki  kumleta  Lowassa  CHADEMA  Lakini nilikuwa  na  misimamo  yangu  ambayo  ilitufanya tusielewane.
 9. Baada  ya  Lowassa  kukatwa  pale  Dodoma, Gwajima ambaye  ni  mshenga  wa  Lowassa  alinipigia  simu kutaka  kujua  nii  cha  kufanya.
 10. Nilimpigia   Mwenyekiti    Mbowe  kumjulisha  na  tukakubaliana  kupanga  muda wa  kuwasikiliza.
 11. Kabla  ya  kuanza  kuwasikiliza, msimamo  wangu  ulikuwa  ni  kumtaka  Lowassa  kwanza  atangaze  kuhama  chama, aweke  wazi  ni  chama  gani  anaenda  na  ajisafishe  juu  ya  tuhuma  zake
 12. Tangu  akatwe  jina, Lowassa  hakutangaza  kujitoa  CCM  na  wala  hakujisafisha  na  tuhuma  zake, kitu  kilichonifanye  nitofautiane  naye.
 1. Niliwauliza  wanachadema  wenzangu  kuwa  Lowassa  anakuja  kama  Mtaji  au  Mzigo?
 2. Swala  sio  urais  kama watu  wanavyozusha, mimi  nilikuwa  nataka  mgombe  mwenye  uwezo  na  sifa  ambaye  ataweza  kuitoa  CCM.  Sikuwa  na  tamaa  ya  urais  kama  watu  wanavyosema
 3. Tangu  Gwajima  atupe  taarifa  za  ujio  wa Lowassa, Swali  langu  la  Lowasssa  kuwa  Mtaji  au  mzigo  halikuwahi  kujibiwa.
 4. Nilitaka  kujua  ni  mtaji  gani  lowassa  atakuja  nao  na  ni  viongozi  gan  atakuja  nao.
 5. Nilijibiwa  kuwa  anakuja  na  wabunge  50  wa  CCM, wenyeviti  22  wa  mikoa  na  wenyeviti  80  wa  wilaya.
 6. Baada  ya  ahadi  hiyo, nilitaka  sasa  nipewe  majina  ya  hawa  watu  lakini  mpaka  tarehe  25  july  sikupewa  hayo majina
 7. Wenzangu  waliniambia  kuwa  tarehe  27  niitishe  kikao  cha  dharura  ila  niligoma  kwa  sababu nilikuwa  sijapewa  haya  majina
 1. Ndani  ya  kikao  hicho tulianza  kwa  mabishano  makali  kati  yangu Mbowe, Lissu  na  Gwajima, viongozi  wenzangu  ni shahidi  na  mungu  anajua. Msimamo  wangu  ulikuwa ni  uleule  kujua  mchango  wa  Lowassa
 2. Kikao  kile  kikavunjika, baadae  tukaingia  kamati  kuu  lakini  bado  msimamo  wangu  ulikuwa  ni  uleule.
 3. Baadae  nikaandika  barua  ya  kujiuzulu. Profesa  Safari  aliichana  ile barua.
 4. Cha  kusikitisha  ni  kuwa  Kesho  yake  picha  zikaanza  kusambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  lowassa  japo  viongozi  wangu  walizikana  zile  picha.  Kibaya  ni  kuwa  viongozi waliuficha  ukweli
 5. Kesho  yake  niliandika  tena  barua  rasmi  ya  kujiuzulu.
 6. Baada  ya  pale  zikaanza  propaganda  za  uongo  zikimuhusisha  hadi  mke  wangu  eti  kanizuia.
 7. Naomba  watanzania  wajue  kuwa  mke  wangu  hakuwahi  kunizuia  kwa  lolote, lakini hata  angefanya  hivyo  sio  mbaya  maana  hata  yeye  ni  mwanaharakati  mwenye  uchungu  na  nchi  hii.
 8. Mke  wangu  aliwahi  hadi  kuumia  wakati  akipigania  ukombozi  wa  nchi  hii…..Lakini  sio  mbaya, familia  yangu  imezoea  propaganda.
 9. Kikubwa  katika  harakati  ni  credibility  ambayo  lazima  uilinde  na  mimi  sitaki  jina  langu  liharibiwe  na  ni  haki  yangu.
 10. Maslah  mapana  ya  taifa  ndiyo  yaliyotufikisha hapa  na  sio  maslahi  binafsi.
 11. Lowassa  na  wapambe  wake  ni  waongo  maana  hakuna  hata  kipengele  kimoja  walichokitekeleza.
 12. Tulitaka  hao  wabunge  50  waje  kwanza  kabla  ya  mchato  wa  uteuzi  ccm
 13. Napinga  kuchukua  makapi  ya  CCM  kuyaita MTAJI.
 14. Mtu  kama  Sumaye  ni  FISADI  na  nilikuwa  siongei  naye
 1. Sumaye  aliwahi  kusema  CCM wakimchagua  Lowassa  atahama  chama. Leo  Lowassa kawaje  msafi??
 2. Tulitaka  Mtaji  toka  kwa  Lowassa  na  sio  MAKAPI
 3. Wenyeviti  walioletwa  na  Lowassa  ni  MZIGO  na  namjua  vizuri. Akithubutu kunijibu  ntamwaga  UOZO  wake  wote
 4. Nani  asiyejua  Guninita  pia  ni  mzigo??
 5. Nawataka  viongozi  wangu  wanijibu  ni  mtaji  upi  walioupata  toka  kwa  Lowassa.
 6. Mimi  ni  Padri  Mstaafu, sipendi  siasa  za  uongo.
 7. Ukisema  unataka  kuiondoa CCM  ni  lazima  ujikumbushe  misingi  ya  CHADEMA
  ambayo  ilikuwa  ni  uadilifu. Leo  chadema  hii ina  Uadilifu  gani??
 8.  Namshangaa  sana  Lowassa eti  kusimama  mbele  ya  watu  akijinasibu  kuwa ni  msafi…..kwamba  mwenye  ushahidi  aende  Mahakamani. Ni  dhambi  kupotosha  watu.
 9. CCM    hawana  ujasiri, ni  waoga  na  ndiyo  maana  wamewalea  watu  kama  akina  Lowassa
 10. Ukitoa  kinyesi  chooni  na  kukipeleka  Chumbani maana  yake  hata  chumba  chako  ni  CHOO  na  kitakuwa  kinanuka  zaidi  kulicho  choo  cha  kawaida
 11. Mimi  nilikuwepo  wakati  sakata  la  Richmond  likijadiliwa. Mimi  nina  ugomvi  wa  muda  mrefu  na  Lowassa.
 12. Mwaka  2010  mimi  nilimtaka  Lowassa  atangaze  Richmond  ni  ya  nani.
 13. Leo  tena  namtaka  Lowassa  atoke  hadharani  atangaze  Richmond  ni  ya  nani Unaposema  ni  ya  mkubwa, atuambie  mkubwa  gani
 14. Ukitaka  kuijua  Richmond  rejea  Ripoti  ya  Mwakyembe. Nampongeza  Mwakyembe  na  Sitta  kujitokeza  hadharan  kuusema  ukweli.
  47. Siku  moja  kabla  ya  ripoti  kusomwa, nililetewa  Rushwa  ya  milioni  500  ili  tukaupindishe  ukweli  bungeni  lakini  nilikataa
 15. Ripoti  ya  mwakyembe  iliamua   mambo  mawili,  moja; Lowassa  ajipime  au  bunge  lijadili  na  lichukue  ripoti.  Lowassa  kuona  hivyo  akaamua  kukimbilia  kujiuzulu  kukwepa  aibu  ya  kung’olewa  na  bunge

49:  Lowassa  haaminiki, ni  muongo  na  hastahili  kuwa Rais  wa  nchi….

 1.  Lowassa  ni  FISADI  na  kama  mimi  ni  muongo  ajitokeze  hadharani  akanushe
 2. Anasema  Lowassa  ataleta  maji, mbona  jimbo  lake  la  Monduli  halina  Maji???
 3.  Mnasema  Lowassa  kaanzisha  shule  za  kata, hivi  mnajua  msingi  wa  shule  za  kata?  waandishi  rudini  shule  mkajifunze  upya.
 4. Nilifanikiwa  kuijenga  Chadema  na  ikawa  tumaini  jipya  la  watanzania…..Vijana  wangu  wa  Chadema, naomba  niwe  mkweli  propaganda imekivamia  chama.
 1.  Inasikitisha  kuona  CHADEMA  inajaza  mabasi  pale  jangwani  badala  ya  watu…..alafu  mnawadanganya  watu  eti  ni   MAFURIKO
 2.  CHADEMA  ya  kipindi  changu  ilikuwa  inakemea  Rushwa. Niambien  leo  chadema  watasema  nini  kwenye  majukwaa?
 3. Mnaomtetea  Lowassa  na  nyie  jitokezen  hadharani…mimi  nasema  kwa  sababu  nina  ushahidi  na  sio  lazima  ushahidi  huu  niupeleke  mahakamani.
 4. Wenye  uwezo  wa  kumpeleka Lowassa  Mahakamani  ni  Serikali, na  mwakyembe  alisema  juzi  kuwa  kesi  ya  jinai  haina kikomo, mtu  anaweza  kushitakiwa  muda  wowote
 5. Sitaki  kuingila  swala  la  Babu  Seya, lakini  waliolawitiwa  ni  watoto  waliokuwa  chini  ya  umri. kwa  nini  haki  yao  ipotee?
 6.  Rais  hana  mamlaka  ya  kumtoa  Babu  Seya. Lowassa  asiwadanganye.
 7.  Kuhusu  swala  la  Masheikh, Sumaye  ndiye  aliyeamuru  mapolisi  wavamie  misikiti  wakiwa  na  mbwa……Watanzania  msikubali  kudanganywa. hizo  ni  propaganda  za  wasaka  urais
 8. Masikubali  Rais  Muongo  na  mimi  naapa  ntapiga  kelele  kila  kona  kumpinga  Lowassa.
 9. Lowassa  alipokuwa  waziri  mkuu, matatizo  yanayotokea  leo  hayakuwepo?  mapigano  ya  wakulima  na  wafugaji  hayakuwepo?
 10.  Lowassa  akiwa  waziri  mkuu  alisababisha  migogoro  mizito  sana  kati  ya monduli  na  karatu.  Rais  wa  aina  hii  wa nini?
 11.  Naomba  nisiongee  mengi  kwa  sababu  ntakosa  ya kusema  siku  nyingine…..Nawataka  Lowassa  na  Sumaye  wajitokeze  kunijibu.
 12. Siku  nyingine  ntakuja  kuongelea  kuhusu  hisa  za  Lowassa  kwenye makampuni
 13. Nahitimisha  kwa  kusema  kuwa  Nimestaafu  siasa  na  sina  chama  lakini  nina  nchi, hivyo  ntaendelea  kuwatumikia  watanzania  kwa  jinsi  mungu  alivyonipa  vipawa
 14.  Sijasema nitajunga na chama gani. Narudia  tena, Sina  chama na  sitajiunga  na  chama chochote. Nitabaki kusimamia ukweli ninaouamini

Waandishi  wanauliza Maswali:

Mwandishi:  

Umesema  ujiungi  na  chama  chochote, utawasaidiaje  watanzania?

Rais  gani unamuunga  mkono?

-Mwandishi  Guardian:  

Ulisema  Lowassa  atakuwa  assert  kama  atakuja  na  wabunge  na  hao  wenyeviti.  Je  angekuja  kama  assert  ungeyasema  haya  yote?

-Mwandishi  binafsi:  

Umesema  na  Chadema  ni  makapi?  Mwaka  1995  Uliihama  CCM, Je  na  wewe  ni  KAPI?

-Mwandishi-Azam:  

Umetangaza kustaafu  siasa, lakini  bado  unakadi  ya  CCM  na  CHADEMA?  Je  utazirudisha?

-Mwandishi  Blog:  

Unaonekana baada  ya  CHADEMA  kukutosa  ndo  maana unamshambulia  Lowassa, je  ni  kweli?

Majibu:

 1. Kadi  ni  mali  zangu  na  siwezi  kuzirudisha. Ya  chadema  nimeilipia  miaka  20.
 2. Kuhusu  urais, mimi  sijagombea  urais  na  sikuchukua fomu.  sasa  kwa  nini  nikasirike  kisa  wamempa Lowassa? Sina  ugomvi  na Mbowe

Mambo sita kutoka kwenye hotuba ya Dr Slaa ambazo zitashusha integrity yake

 1. Alikuwa mtu wa kwanza na mstari wa mbele kumelta LOWASSA CHADEMA hivyo alikuwa tayari kumleta LOWASSA CHADEMA huku akijua na kuamini kuwa LOWASSA ni fisadi na kwa hiyo sasa akimshambulia ni kwa vile matarajio yake hayakutimia. No 8-11
 2. Alukuwa after mtaji wa wabunge 50, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya wa CCM na wala sio ufisadi wa LOWASSA no 11-18, 31, 35
 3. Hana uhakika kama LOWASSA ni fisadi na ushahidi wake ni wa kimazingira tu kitu ambacho inaweza kuwa fikra zilizojificha ndani ya kuchafuana kwenye siasa. No. 11,12,44,45
 4. Shutuma ni zile zile kwa mtindo uleule wa CCM makundi, 46,47… Inatufanya tuamini kuwa Dr Slaa, Nape, Kinana na Mwakyembe wanachezea timu moja japo Dr Slaa yeye hajavaa jezi tu.
 5. Mashambulizi yote ya DR Slaa kwa CHADEMA na Lowassa inaendana na stori ya Sungura ya “Sizitaki mbichi hizi” Kwa vile yeye kakosa kuipeperusha bendera ya Urais kupitia CHADEMA/UKAWA 25 Octoba 2015 sasa anabwaga manyanga ili wote wakose.
 6. Dr Slaa ni Mwongo na wala haijui Monduli. Alete ushahidi kwamba Monduli haina maji, no 51. Mara asema bado kusema atakuwa chama gani na wakati mwingine anasema hatajihusisha na siasa za vyama. Time will tell No 67. LOWASSA Hakusema atawatoa Babu Sea na Mashehe wa Zanzibar, alisema atatumia sheria na utawala bora kulishughulikia masuala hayo . no. 58, 60. Lowassa hakuletwa ba Gwajima bali yeye mwenye ndie aliyemtafuta Lowassa kuanzia Mei 2015

Leave your comment about Hotuba ya Dr Slaa Serena Hotel 1 Septemba 2015 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here