HOTUBA YA DR SLAA YA KUNG’ATUKA SIASA ZA VYAMA SERENA HOTEL 1 SEPTEMBA 2015

0
817
Dr Wilbroad Slaa Akitangaza Kuachana na Sisa za Vyama

Mambo kumi (10) ambazo zitashusha Heshima ya Dr Slaa

  1. Alikuwa mtu wa kwanza na mstari wa mbele kumelta LOWASSA CHADEMA hivyo alikuwa tayari kumleta LOWASSA CHADEMA huku akijua na kuamini kuwa LOWASSA ni fisadi na kwa hiyo sasa akimshambulia ni kwa vile matarajio yake hayakutimia.
  2. Alukuwa after mtaji wa wabunge 50, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya wa CCM na wala sio ufisadi wa LOWASSA
  3. Hana uhakika kama LOWASSA ni fisadi na ushahidi wake ni wa kimazingira tu kitu ambacho inaweza kuwa fikra zilizojificha ndani ya kuchafuana kwenye siasa.
  4. Shutuma ni zile zile kwa mtindo uleule wa CCM makundi, Inatufanya tuamini kuwa Dr Slaa, Nape, Kinana na Mwakyembe wanachezea timu moja japo Dr Slaa yeye hajavaa jezi tu.
  5. Mashambulizi yote ya DR Slaa kwa CHADEMA na Lowassa inaendana na stori ya Sungura ya “Sizitaki mbichi hizi” Kwa vile yeye kakosa kuipeperusha bendera ya Urais kupitia CHADEMA/UKAWA 25 Octoba 2015 sasa anabwaga manyanga ili wote wakose.
  6. Dr Slaa ni Mwongo na wala haijui Monduli. Alete ushahidi kwamba Monduli haina maji. Mara asema bado kusema atakuwa chama gani na wakati mwingine anasema hatajihusisha na siasa za vyama. Time will tell. LOWASSA Hakusema atawatoa Babu Sea na Mashehe wa Zanzibar, alisema atatumia sheria na utawala bora kulishughulikia masuala hayo. Lowassa hakuletwa ba Gwajima bali yeye mwenye ndie aliyemtafuta Lowassa kuanzia Mei 2015
  7. Yeye huwa anasema ni mla mihogo, gharama ya kurusha matangazo kwa channel za Star Tv, Azam two, channel10 na radio kwa saa nzima kalipiwa na nani?
  8. Kwanini hakumtaja aliejaribu kumpa rushwa ya milion 500?
  9. Kwanini aitishe press conference Tarehe 1, Septemba 2015 baada ya sheria ya makosa ya mtandao kuanza kufanya kazi?
  10. Anasema alijiuzulu tangu Mwezi wa 7, je mbona hakuzungumzia mshahara aliouchukua mwezi uliopita wa Agosti?

Leave your comment about HOTUBA YA DR SLAA YA KUNG’ATUKA SIASA ZA VYAMA SERENA HOTEL 1 SEPTEMBA 2015 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here