Je wajua? Osama Bin Laden Amekufa!

1
1726
Osama Bin Laden Amekufa
Osama Bin Laden Amekufa

Osama Bin Laden – Gaidi Mkubwa Kutokea Duniani Amekufa

Osama Bin Laden Amekufa
Osama Bin Laden Amekufa

 

Gaidi mkubwa kabisa kutokea duniani Osama Bin Laden amekufa baada ya shambulizi la kushtukiza lililofanywa na majeshi ya kimarekani katika nyumba yake ya ghorofa tatu. Taarifa za kiitelijensia zilisema kwamba Osama alikuwa akiishi katika ghorofa ya tatu ya ghorofa hiyo. Taarifa hiyo ni ya kweli na hayo yalidhibitishwa baada ya majeshi ya marekani kumkuta pamoja na mke anayeaminika kuwa ni mke wake mdogo ambaye pia alimtumia kama kinga yake ya kibinadamu. Mashambulizi hayo kushtukiza  bila kuhusisha jeshi la Pakistani yalifanywa na majeshi ya kimarekani kwa kutumia helkopta nne ambako moja ambayo ilipata hitilafu.

“Haki imetendeka”

 

 

Nyumba aliyoishi Osama haikuwa na mawasiliano yeyote ya simu wala intaneti na ilijengwa mwaka 2005 umbali wa kama maili 60 kutoka katika mji wa Islababad maalum kwa ajili ya Osama. Jengo hilo liligharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni moja (US$ 1,000,000)

Iliwachukua dakika 40 kupambana kwa risasi za moto kabla ya kumuua Osama Bin Laden –

Lakini watu wengi wanajiuliza imekuwaje Wapakistani na hasa serikali na jeshi la Pakistani lisijue kuwa mtuhumiwa namba moja wa Ugaidi duniani alikuwa anaishi Pakistani.

Rais wa Aghanistani katika hotuba yake amesema kwamba Osama amewauwa baba, mama, watoto na ndugu zetu wengi . Kifo cha Osama kimeipatia Alkaeda hatma mbaya. Tutaendelea na kupambana kwani vita vya Ugaidi bado havijaisha.

Osama amezikwa kwa heshima zote za kiislamu kwa kuvishwa vasi la mazishi jeupe na kuteremshwa taratibu chini ya bahari. Video zimechukuliwa za tukio lote na zitaonyeshwa ili watu wote waone.

Taarifa za kiitelijensia shirika la kipelelezi la CIA la marekani zinadai kuwa wafuasi wakereketwa wa Osama wanapanga njama za kulipisa kisasi kifo cha mpendwa wao na kiongozi wao Osama Bin laden muda wowote kuanzia sasa popote duniani. Kwa hiyo watu.

Leave your comment about Je wajua? Osama Bin Laden Amekufa! using the comment form below

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here