Jeshi la Polisi Wanamshikilia Dkt. Louis Shika kwa kuharibu Mnada wa Nyumba za Lugumi

0
16

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa lina mashaka kuhusu uhalali wa udaktari wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa tajiri aliyeshinda katika mnada wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi uliofanyika siku ya Alhamisi kwa kuwa ameshindwa kuonyesha vielelezo vya kuthibitisha elimu yake ya kiwango cha Ph.D. Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa wanaendelea na upelelezi dhidi ya mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Dkt. Lius Shika.

Jeshi hilo la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linamshikilia mtu huyo aitwaye Dkt. Louis Shika kwa tuhuma za kuharibu mnada wa hadhara wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo alishinda mnada wa nyumba zote tatu zenye thamani ya shilingi bilioni tatu nukta tatu lakini alipotakiwa kulipa asilimia 25 ya gharama hiyo alishindwa.

Image may contain: 1 person, standing

Leave your comment about Jeshi la Polisi Wanamshikilia Dkt. Louis Shika kwa kuharibu Mnada wa Nyumba za Lugumi using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here