Rais wa Colombia Juan Manuel Santos Apewa Nishani ya Amani ya NOBEL

0
160

Rais wa Colombia Juan Santos Apewa Nishani ya Amani ya NOBEL 2016
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, amepewa Nishani ya Amani ya NOBEL  iitwayo   NOBEL PEACE PRIZE kwa mwaka huu wa 2016.

Hii ni baada ya kukazania na kufanikiwa kutiwa kwa saini ya mapatano kusitisha viata vya wenyewe kwa wenyewe na kundi la msituni la FARC ambalo limepambana na serikali ya Colombia kwa zaidi ya miaka 50. Makubaliano hayo yalifikiwa 7 Octoba 2016 na Congress ya Colombia baada ya kupigiwa kura ya maoni mara mbili.

Vita hivi viliondoa maisha ya watu zaidi ya 220,000 na takribani watu milioni 6 kuyakimbia makasi yao bila ridhaa yao.

Huu ni ujasiri mkubwa sana kwa mtu aliyekikalia kiti cha keko ya Taifa kukubali win win na waasi au siku hizi wakiiutwa magaidi. Huyu anaweza kuwa ni Nelson Mandela wa pili kutokea duniani, sio rahisi hata katika mataifa yaliyostaarabika kuwakubali waasi na kukaa kiti kimoja na kukubalian kuongoza nchi pamoja.

Natamani wapenda amani pengine duniani waige mfano huu. Asad wa Syria ajifunze kutoka kwa Santos. Kukimbilia kuwaita wanaotetea haki zao magaidi au waasi sio muda wake kwenye karne hii. WIN WIN ndio njia pekee ya kudumisha amani katika nchi na Duniani

Hongera Juan Manuel Santos,

Leave your comment about Rais wa Colombia Juan Manuel Santos Apewa Nishani ya Amani ya NOBEL using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here