Kanisa Katoliki Lalipuliwa kwa Bomu Arusha

2
1422
Majeruhi wa Kanisa Katoliki Akihudumiwa Mount Meru Hospital Arusha
Majeruhi wa Kanisa Katoliki Akihudumiwa Mount Meru Hospital Arusha
Majeruhi wa Kanisa Katoliki Akihudumiwa Mount Meru Hospital Arusha
Majeruhi wa Kanisa Katoliki Akihudumiwa Mount Meru Hospital Arusha

Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa kumetokea mlipuko mkubwa unaosadikiwa kuwa kusababishwa na bomu la kurushwa wakati ibada ilipokuwa ikiendelea katika kanisa jipya la parokia ya Olasiti, jijini Arusha na kuua watu wanne na majeruhi kadhaa.

Kanisa hilo lilikuwa linazinduliwa rasmi na Mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi wa Papa kutoka Vatican. Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa kutoka mataifa mbalimbali.
Majeruhi wa Kanisa lililolipuliwa Kwa Bomu Arusha
Majeruhi wa Kanisa lililolipuliwa Kwa Bomu Arusha
Mtoto mmoja ameeleza kuwa aliona watu waliokuwa kwenye mini bus (Hiece) wakirusha kitu kuelekea kwenye mkusanyiko wa wakristo waliokuwepo kwenye ibada.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa na takriban watu wanne wamepoteza maisha.  Muda huu vyombo vyote vya usalama vipo eneo la tukio vikihakikisha usalama zaidi.

Kuna taarifa ya milipuko mingine, haijulikani kama ni ya washambuliaji au ya polisi, mbali na eneo la ibada.

Kwa update zaidi sikiliza Radio Maria http://streema.com/radios/play/6848.

Leave your comment about Kanisa Katoliki Lalipuliwa kwa Bomu Arusha using the comment form below

2 COMMENTS

 1. Polisi nchini Tanzania inawashikilia watu nane kwa madai ya kuhusika na mlipuko wa bomu siku ya jumapili katika Kanisa la Katoliki Mfanyakazi la Olasit jijini Arusha.

  Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.

 2. Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo maneno kwenye eneo la ajali, Lema anasema bomu lililolipuliwa limetokana na sababu za kisiasa na lazima hatua kali zichukuliwe kwa wahusika naye mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo anasema Lema aache siasa hapa na asaidie kuokoaMagessa baadaye anaondoka huku akizomewa.

  Mulongo ameagiza magari ya polisi hapa Mount Meru ili ‘kutuliza’ fujo’ zinazoanza kushabikiwa na wanasiasa.
  Kwa upande wa majeruhi, wengi wao ni watoto.

  Taarafa za kipolisi zinasema kuwa watu watatu wamethibitishwa kupoteza maisha, inakuwa vigumu kutambua idadi kamili maana majeruhi wamesambazwa hospitali tatu hapa mjini.
  Watu wawili wamekamatwa tayari kuhusiana na tukio hili hadi sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here