Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar

1
1771
Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar
Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar
Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar
Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar

Kanisa kubwa la kipentekoste la PAG lachomwa moto mjini Zanzibar. Kanisa hilo lipo eneo la kariakoo Zanzibar. Ikumbukwe kwamba hili ni Kanisa mama na kanisa kubwa la kilokole kuliko yote hapa Zanzibar lenye takribani watu 500-800. Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia jumapili  leo (27/5/12) masaa ya saa nne usiku hivi wakati Mchungaji pamoja na kikundi cha vijana wakifanya maombi. Kwa ghafla lilikuja kundi la watu zaidi ya 100 na kuanza kurusha mawe na kubomoa kanisa. Mchungaji na vijana waliokuwepo hawakuumia baada ya kujikinga ndani ya vyumba vya kansani.

Viti na milango kuchomwa moto
Viti na milango kuchomwa moto

Baadhi ya vitu vilivyoharibiwa ni;

  1. Viti na milango kuchomwa moto,
  2. Paa limeungua lakini bati hazikuadhilika sana zaidi ya nyaya za umeme kuungua
  3. Gari la Mchungaji na Askofu Kaganga limechomwa moto
  4. Ukuta wa kuzunguka kanisa umebomolewa pamoja na madirisha na kuta za kanisa pia zimebomolewa
  5. Hakuna aliyeumia
Chanzo kikuu ni kukundi kinachoojiita “kikundi cha Uamsho” kinachoongozwa na jopo la mashehe (wengi wenye asili ya kiarabu) kinadai nchi yao ya Zanzibar na kuvunjika kwa muungano. Kikundi hiki kimekuwa maarufu hapa Zanzibar na kimekuwa kikifanya mihadhara mingi na maandamano bila ya kuingiliwa na serikali lakini jana mmoja wa vingozi wa kikundi alikamatwa  na ikawa ndicho kichocheo cha vurugu hizi.
Makanisa Sasa Kuwa Hatarini Zanzibar kwa Sababu Ya Chuki ya Kidini
Makanisa Sasa Kuwa Hatarini Zanzibar kwa Sababu Ya Chuki ya Kidini

Kabla ya tukio hili baadhi ya makanisa, hasa nje ya mji yameshashambuliwa lakini ilikuwa na vigumu kulifikia kanisa kama hili la kariakoo ambalo lipo katikati ya mji. Pia zama hizi kumekuwepo na ongezeko la vitendo vya chuki zidi ya wabara hasa sababu wengi wanaonekana kuwa wakristu. Hatari inaongezeka  kwa wanawake ,  wamekuwa wakitupiwa maneno na hata kupigwa  wanapopita baadhi ya sehemu. Chuku hasa ni wabara kuonekana wanaeneza ukristu kupitia kwenye muungano.

Leave your comment about Kanisa Kubwa la Kipentekoste Lachomwa Moto Zanzibar using the comment form below

1 COMMENT

  1. Na kwnn mnataja makanisa tu misikiti hamuitaji, na kwnn wakristo watoke tanganyika kueneza ukristo Zanzibar? Wakati kila leo tunaambiwa wakristo Zanzibar walikuepo, hii ni husda yao tu makafiri dhidi ya waislamu, na hawataridhika milele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here