Kati ya Alvaro Morata na Romelu Lukaku, Nani Zaidi?

0
320
Alvaro Morata VS Romelu Lukaku

Msimu ujao utashuhudia sura nyingi mpya katika ligi maarufu duniani ya Uingereza ijulikanayo kama EPL wakizitetea kwa ari mpya timu zao ili kutetea first eleven ambayo ndiyo itakayowapa nafasi ya kujulikana na kupanda bei zaidi. Mojawapo ya sura mpya katika timu na pia katika ligi ya uingereza msimu ujao ni Alvaro Morata aliyekuwa Mshambuliaji wa Mabingwa wa Hispania na Ulaya (UEFA Champions) klabu ya Real Madrid

Kwa upande wa ugungaji na kasi ya mpira Lukaku anachukua nafasi ya juu kabisa kwani katika msimu uliopita aliweza kufunga magoli 40 katika mechi 58 alizocheza. Lukaku anao uwezo wa kumalizia kufunga na ndio maana ana magoli mengi tofauti na Morata. Lukaku kafunga magoli 25 katika mechi 37 za EPL alizocheza.

Lukaku ni mmojawapo ya wachezaji 10 bora duniani waliofunga magoli mengi chini ya umri wa miaka 23 kama inavyoonyeshwa kwenye takwimu hizi

  1. Ronaldo Luís Nazário de Lima wa Brazil– 194
  2. Raúl González Blanco wa Hispania – 145
  3. Lionel Andrés “Leo” Messi wa Argentina– 127
  4. Sergio Leonel “Kun” Agüero wa Argentina – 124
  5. Romelu Menama Lukaku Bolingoli wa Ubelgiji – 119
  6. Michael James Owen wa Uingereza – 111
  7. Cristiano Ronaldo dos Santos wa Ureno – 97
  8. Fernando José Torres Sanz  wa Hispania – 87
  9. Wayne Mark Rooney  wa Uingereza – 94
  10. Luis Alberto Suárez Díaz wa Uruguay – 77

Kwa upande wake Alvaro Morata ni mchezaji mwenye ujuzi na uwezo wa kucheza kwenye pressure kubwa na kupangua defense. Alvaro kwa aliweza kufunga magoli 27 katika mechi 52 alizocheza huku akifunga magoli 15 katika mechi. Morata ana uwezo wa kukaa na mpira na kutengeneza pasi za uhakika tofauti na Lukaku.

Wote kwa pamoja wanasajiliwa kama replacement ya wafungaji wazuri na wenye historia nzuri ya uchezaji. Lukaku anachukua nafasi ya Zlatan Ibrahimovi? na Morata anachukua nafasi ya Diego Costaaliyeachwa kwa sababu ya kutoelewana na Antonio ConteAlvaro Morata vs Romelu Lukaku StatisticsJe unafikiri Chelsea wameboronga kwa kumwajiri Morata badala ya Lukaku?

Je umadhani Man United wamechemsha kwa kumuajiri Lukaku badala ya Morata? 

 

Leave your comment about Kati ya Alvaro Morata na Romelu Lukaku, Nani Zaidi? using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here