Kiboko – Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani

1
7391
Kiboko - Mnyama Mwenye Domo Kubwa Duniani

Kiboko Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko WoteMnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani ni Kiboko.

Kiboko ndiye mpaka sasa hivi anayeongoza duniani kwa kuwa na mdomo mkubwa. Pia anaongoza kwa kupanua mdomo anapopiga miayo. Mdomo wake unaweza kupanuka mpaka digrii 170 ambayo ni sawa na mstari ulionyooka ukipungua kwa digrii kumi (10) tu.

  • Anakimbia kwa wastani wa kilomita 19 kwa saa akiwa nchi kavu
  • Anaishi miaka 40 -50
  • Dume lina uzito wa ratili 3,300 – 4,000
  • Jike lina  uzito wa ratili 2,900 – 3,300

Mnyama huyu anapatikana sehemu Ngorongoro, Ruaha, na sehemu zingine za Afrika. Kiboko anaishi majini na Nchi kavu. Muda mwingi majini na nyakati za jioni anatoka kwenda kutafuta malisho. Kiboko muda mwingi anapenda kukaa kipweke na kiboko wa kiume ni mzito kuliko wa kike. Kiboko anaweza kufikia tani 2-3 na kumfanya kuwa mnyama wa nchi kavu wa tatu kwa uzito duniani baada ya Tembo na Kifaru. Kiboko pia ni mnyama wa nchi kavu wa pili duniani kwa ukubwa baada ya Tembo. Kiboko anakula tu majani na hivyo kuwa sawa na Ngombe, Mbuzi, Nyati, Swala, Pundamilia, na jamii yote ya wanyama wannaokula majani tu.

Leave your comment about Kiboko – Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani using the comment form below

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here