Kichekesho cha Jaluo na Lugha ya Kiswahili

3
11039
Kichekesho cha Jaluo Anakojoa

Siku moja tulipokuwa tunasafiri kutoka Mwanza kuja Arusha kupitia Magu – Serengeti na ndani ya Gari tulikuwa na Abiria wa kike na wa kiume wakubwa kwa wadogo. Lakini pia kulikuwa na mjaluo mmoja ambaye alikuwa ni mwongeaji sana japo kwa kiswahili cha kijaluo wote tunajua jinsi wajaluo wanayojua lugha ya Kijaluo na Kiingereza lakini ikija kiswahili ni vunja mbavu tu.

Tulipofika makuyuni tuliteremka ili tupate break fupi ya kinywaji na wengine kuchimba dawa. Baada tu ya kuteremka kwenye gari, yule jaluo ghafla wakati ametukabili akasema kwa sauti kubwa

“HAPA NAKOJOA”

Akina mama na watoto wadogo wakakimbia haraka mbali wakijua jaluo anataka kukojoa pale pale, Kumbe yeye alimaanisha eneo lile analifahamu

Leave your comment about Kichekesho cha Jaluo na Lugha ya Kiswahili using the comment form below

3 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here