Kichekesho cha Kiongozi Mkaidi Kuumwa na Nyuki

0
162
Rais wa Kongo Joseph Kabila Aumwa na Nyuki Ikulu

Kiongozi mmoja wa nchi jirani alitembelea kwa kushtukiza seheemu ya kufuga nyuki katika utaratibu wake wa kukagua miradi ya maendeleo.

Alipofika katika lango la kuingilia kwenye eneo lenye mizinga ya nyuki, mlinzi wa zamu akamuambia wageni hawaruhusiwi kuingia humo.

Kiongozi huyo alishangaa halafu akamuangalia kisha akamuuliza.

Kiongozi: “Kwani wewe hunijui kuwa mimi nani? Kabla hajajibu akamtolea kitambulisho chake.

Mlinzi akanyamaza tu na yule kiongozi akaingia ndani. Ndani ya muda mfupi kelel zikasikika kiongozi akilia ‘Nisaidieni, naumwa na nyuki.

Mlinzi: Kwani hao nyuki hawajui wewe nani? kabla hajajibu mlinzi akamwambia waonyeshe kitambulisho chako.

Leave your comment about Kichekesho cha Kiongozi Mkaidi Kuumwa na Nyuki using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.