KITUO CHA LHRC KUMFIKISHA WAZIR MKUU PINDA MAHAKAMANI

0
1038
KITUO CHA LHRC KUMFIKISHA WAZIR MKUU PINDA MAHAKAMANI

KITUO CHA LHRC KUMFIKISHA WAZIR MKUU PINDA MAHAKAMANIKuhusu kumshtaki PM ni kweli draft petition chini ya BRADEA iko tayari kwa kwenda mahakamani by alhamis Mungu akipenda. Tutaitisha press conference.

Hata hivyo tunapambana na kisiki kimoja cha kisheria nacho ni ibara ya 100(1) ijapokuwa ibara ya 100(2) inatupatia ka nafuu kadogo.

Swali la kisheria ni ikiwa hiyo parliamentary immunity inaweza kutumika kama ngao kwa mtu anayevunja katiba waziwazi?

Mfano, mbunge ambaye ni waziri akiwa bungeni na kisha akaagiza wananchi wakiwaona wamachinga wote wawanyang’anye bidhaa zao? au wananchi wakiona mama ntilie wawapore chakula? Au changudoa wakionekana wabakwe?, je bado kauli kama ya huyo waziri itakuwa na kinga? Ndiyo au la?

Kwa ufupi tutataka kwanza mahakama ishughulike na hilo la kinga maana najua tu AG ataweka pingamizi la awali kama ilivyo kwawaida yake. Tutashughulika na hoja hiyo kungali asubuhi kisha tujue kama mahakama ikisema kuwa mhe. Pinda ana kinga ya kutoshtakiwa hata kama amevunja katiba au haki za msingi then tutakwenda kwenye mahakama yetu tuliyoizoea na hapo hakutakuwa na kisingizio kuwa hatuja exhaust local remedies maana mpaka hapo ni ushahidi kuwa tz hakuna hizo local remedies katika hilo. Kwa kuwa haki zinazovunjwa ziko pia kwenye mkataba wa afrika then wembe uliotumika kwenye kesi ya mgombea binafsi ndo utaendelea kutumika.

All in all wanamabadiliko tunaomba majibu kama Kinga ya bunge ina mipaka? Kama ipo ni ipi mipaka yake?

Taratibu tutafika tu.

By the way. Kama kuna anayehitaji ku sign ile petition nyingine ya umma kupinga kauli ya mhe. Pinda, tafadhali tujulisheni. Hadi sasa tunakaribia signature 3000.

Wasalaam
Sungusia LHRC

Leave your comment about KITUO CHA LHRC KUMFIKISHA WAZIR MKUU PINDA MAHAKAMANI using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here