Jana akihutumia umati mkubwa wa wafuasi wa UKAWA katika ofisi za CHADEMA, Kinondoni, Lowassa alimlipua kwa mara ya pili Kikwete kwa kusema kuwa kaharibu uchumi wa nchi
“Rafiki yangu Kikwete kaharibu uchumi wa nchi yetu”
“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.
“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni,” amesema Lowassa.
Amedai kuwa yeye akiingia madarakani atashughulika kwanza na matatizo ya vijana na watanzania wa uchumi wa chini. Alisema ili kufanikisha hayo ataunda serikali rafiki kwa makundi hayo.
Akihutubia kwenye press conference ya kupokelewa CHADEMA mwezi uliopita Lowassa alimplipua Kikwete kwa kusema kuwa alitaka kusitisha mkataba wa Richmond lakini bosi wake ambaye ni Kikwete akamzuia.