Mabalozi Batilda, James Nsekela na Kalaghe Warudishwa Nchini

0
667
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni SefueAkitangaza Kurudishwa kwa Mabalozi
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Akitangaza Kurudishwa kwa Mabalozi, Kufukuzwa kazi, kusimamishwa kazi kwa watumishi wa Serikali Wenye Utendaji Dhaifu

Rais Magufuli ameamuru kurudi haraka nyumbani mabalozi hawa Dr Batilda Buriani, Dr James Nsekela wa Italia na Peter Kalaghe wa Uingereza. Akitangaza hatua hiyo, Katibu mkuu kiongozi Ombeni sefue amesema Batilda na mabalozi wengine watano wamekuwa hawafanyi kazi kikamilifu ya kuiwakilisha nchi kama jinsi majukumu yao yanaavyoeleza.

Sefue amewataka mabalozi hao watatu kuondoka leo hii katika nchi waliko na kurudi Tanzania. Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao.

Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

  1. London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE
  2. Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.
  3. Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.
  4. Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI
  5. Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.
  6. Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

UTEUZI WA BALOZI WA KWANZA NCHINI KUWAIT
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

Leave your comment about Mabalozi Batilda, James Nsekela na Kalaghe Warudishwa Nchini using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here