Magufuli Ateua Mawaziri Wanne wa Wizara Zilizobaki Yumo Prof. Joyce Ndalichako wa NECTA

0
2181
Rais John Pombe Joseph Magufuli Awateua Mawaziri Waliobaki akiwemo Dr Joyce Ndalichako
Rais John Pombe Joseph Magufuli Awateua Mawaziri Waliobaki akiwemo Dr Joyce Ndalichako

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameteua mawaziri na naibu waziri wa wizara zilizobaki bila ya mawaziri kufuatia uteuzi wa awali alioufanya wiki chache zilizopita.

Mawaziri na naibu waziri walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

Magufuli Awateua Mawaziri Wanne akiwemo Dr Joyce Ndalichako wa NECTA
Magufuli Awateua Mawaziri Wanne akiwemo Profesa Joyce Ndalichako Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NECTA
  1. Profesa Jumanne Maghembe – Waziri wa Maliasili na Utalii.
  2. Dr. Philip Mpango – Waziri wa Fedha na Mipango (Baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mbunge).
  3. Mhandisi Gerson Lwenge – Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
  4. Profesa Joyce Ndalichako – Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.(Baada ya kuteuliwa na Rais kuwa Mbunge)
  5. Mheshimiwa Hamad Masauni – Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
  6. Prof. Makame Mbarawa –Kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Katika uteuzi huo, uteuzi wa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ndio wenye kuvuta hisia za wengi ukichukulia kwamba wizara hii iliongoza kwa kuboronga kwenye utawala wa awamu ya nne chini ya Dr. Shukuru Kawambwa. Aidha Profesa Joyce Ndalichako alikuwa ndie Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa -NECTA kwa miaka minne wakati wa uongozi wa Dk Jakaya Mrisho Kikwete ambae kwa wakati fulani uliingia kwenye mvutano na wizara juu ya mfumo mpya wa usahihishaji na utoaji maksi kwa mtindo wa GPA.

Profesa Ndalichako aliamua kuchukua likizo ya masomo baada ya kukataa mpango wa wizara ya elimu ya kushusha grade za matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 (ambao yeye aliuita ni wa kisiasa zaidi na haukuwa na tija katika kuboresha elimu) ambapo kiwango cha kufeli kilikuwa kubwa sana kupita miaka ya nyuma yake. Serikali iliilazimisha NECTA kushusha grade kwa kutumia fomula mpya ili ufaulu upande na kufuta aibu ya maelfu ya wanafunzi kufeli. Mvutano huu ulimpelekea Dr Ndalichako kujiuzulu na kurudi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano ni kudhihirisha kuwa Dr Joyce Ndalichako anafaa kuleta mageuzi kwa kuusuka upya mfumo wa elimu Tanzania na kuondoa ombwe la elimu kushuka nchini.

Leave your comment about Magufuli Ateua Mawaziri Wanne wa Wizara Zilizobaki Yumo Prof. Joyce Ndalichako wa NECTA using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here