Magufuli – Dereva Mahiri Ndani ya Garimoshi

0
770
Magufuli ni sawa na dereva mahiri ndani ya garimoshi

Haina maana ukibadilisha dereva wa treni lile la zamani linalotumia kuni litaweza kukimbia kilomita 500 kwa saa kama lile la umeme.

Tunaposema gari moshi haliwezi kukimbia kilomita 500 kwa saa tuna maana mfumo wake wa utendaji kazi ndio unaamua likimbie kilomita 80 kwa saa tu na sio 500

Haimaanishi pia tukibadilisha Rais ndani ya CCM Tanzania itapata mabadiliko tunayoyataka

Tuna maana huo mfumo wa utendaji ndani ya CCM ndio ambao hauruhusu mabadiliko watakayo Watanzania.  Mfano mzuri ni wakati wa kutunga katiba mpya.

Dereva anaweza kuwa ni yule yule wa garimoshi akipewa treni ya umeme ataliendesha kwa kasi ya kilomita 500 kwa saa

Mgombea Urais anaweza kuwa ni yule yule wa CCM lakini akiwa ndani ya chama kipya chenye fikra mpya na mfumo mpya wa kiutendaji anaweza kulipeleka Taifa kwenye mabadiliko tutakayo na mchakamchaka wa maendeleo.

Magufuli ni sawa na dereva mahiri ndani ya garimoshi

 

Leave your comment about Magufuli – Dereva Mahiri Ndani ya Garimoshi using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here