Majibu ya Dr Slaa kwa Tundu Lissu na Rose Kamili

0
988
Dr Slaa ajibu mapigo ndani ya Star TV 5 Septemba 2015

Kilichonivutia pia ni kukubali indirectly kuwa kapokea mshahara wa agosti na pia kutojibu kabisa suala la yeye kufukuziwa nje na H… wake maana siwezi mwita mke au mchumba wakati mke wake wa ndoa bado yupo.

Kakataa pia kutoa ushaihidi wa ufisadi wa Lowassa akimtaka aende mahakamani. hici huwa ni mtuhumiwa ndie anayeenda mahakamani au anayemtuhuu ndie anatakiwa kumpeleka mtuhumiwa mahakamani?

Aliendelea kukiri pia kuwa sababu kuu ya kudai kuwa Lowassa ni fisadi ni kwa sababu ya Katiba katika ibara ya 52 kinachosema kuwa Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na pia alienda kinyume na taratibu za manunuzi na maamuzi ya baraza la mawaziri. hizo ndizo sababu za kudai lowassa fisadi ndio maana wanaogopa kwenda mahakamani

Kakiri pia kuwa anashirikiana na Dr. Mwakyembe kuweka data zake sawa
Kakiri pia kuwa anashirikiana na polisi…… na usalama wa …. kuhakikisha usalama wake unakaa vizuri na kwamba walimlinda vizuri alipokuwa likizo Serengeti akiangalia wanyama

Kamlipua pia Magufuli bila kujua kwa kudai kuwa mgombea anatakiwa kupimwa kwa kuangalia jimboni mwake kafanya nini?

Kajibu vizuri pia shutuma za mke wake wa ndoa kuwa hawezi kuwalea wazee wa Rose Kamili ila hakujibu shutuma za kwamba yeye ni mla mihogo huku watoto wake na Josephine Mushumbusi ambao sio wazee wakisoma huku wakila bata Uganda.

Hakujibu pia shutuma za Rose Kamili kuwa yeye ni mwongo kwa kuishutumu serikali kumuwekea pingamizi la talaka huku akijua ni Rose Kamili aliyemuwekea ili kulinda maslahi ya mali za familia dhidi ya JMushumbusi

Alijibu vyema pia kuwa yeye na Gwajima ni maswahiba wakati Gwajima na Lowassa pia ni maswahiba.

Alijibu vyema shutuma za Tundu Lisu kuwa aliteuliwa na kamati kuu february 2015 kuwa mgombea wa CHADEMA na kuweka bayana ya moyoni ambayo hakusema kwenye Press Conference ya Serana kuwa naye ana moyo wa Nyama, ameumia sana mtu wa nje kuja kuchukua nafasi yake pamoja na kwamba yeye alijiandaa kwa muda mrefu na pia kwa gharama za kupelekwa nje kwenda kujifunza na kuchukua uzoefu wa kuongoza nchi kama presidenti.

Alikiri pia kuwa Magufuli fisadi na sio tu aliuza nyumba za serikali bali pia alimuuzia rafiki wake wa…. nyumba kinyume na taratibu. Alihitimisha kwa kuwaasa watanzania kumchagua Magufuli mwenye ufisadi mdogo kuliko Lowassa mwenye ufisadi mkubwa

Akatuachia maswali makuu mawili
1. Kipimo cha Lowassa ni fisadi mkuu na Magufuli ni fisadi mdogo anayo Dr Slaa tu?
2. Lowassa ndani ya UKAWA isiyo na ufisadi na Magufuli ndani ya CCM iliyojaa mafisadi nani bora?

Leave your comment about Majibu ya Dr Slaa kwa Tundu Lissu na Rose Kamili using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.