Majina Maarufu Yenye Maana Mbaya

0
623

Je wewe unajua maana ya jina lako? Je wewe una mtoto ambaye umempa moja ya majina usiyojua maana yake? Je wewe ni mzazi mtarajiwa na unapata shida kumpa motto wako jina?

Ushauri wa bure, tafuta maana ya jina kabla hujampa motto wako jina kwani uridhi wa kwanza wa mzazi kwa motto ni jita. Hii nio zawadi pekee mzazi anampa mtoto pale tu anapoingia duniani kwa mara ya kwanza.  Ukimpa mtoto jina baya litamsumbua sana maishani hasa atakapokuwa mkubwa na saa nyingine itamgharimu kuchukua hatua za kisheria za kubadilisha jina.

Njia rahiu ni hii

1.       Mpe mtoto jina lenye maneno rahisi na yanayojulikana hata kabal ya kwenda kwenye kamusi. Na kina iendane na maono uliyo nayo kwa mtoto wako

2.       Kama utampa mtoto jina gumu na geni uliza kwa wenye lugha, kwa majina ya kiingereza ni rahisi kwani internet ina tovuti nyingi na kamusi za majina ambazo takribani kila jina la kiingereza limepewa maana yake

Ifuatayo ni baaadhi ya majina na maana zake ambazo sio nzuri sana

Cecilia – Neno la kilatini caecus ikiwa na maana ya Kipofu (blind)

Gideon – Jina la kiebrania likiwa na maana ya mharibifu (destroyer)

Kennedy – Jina la kiscottish hass kigaeliki au kiseltiki likiwa na maana ya Kichwa kilichopondeka (a deformed Head in Gaelic or Celtic language)

Cameron  – Pua iliyopinda au kama ndoano (Crooked nose)

Calvin – Limetokan a na neon la kilatini la Bald likiwa na maana ya kichwa bila nywele au ikiwa na nywele pungufu au Kipara

Lea. – Neno la kiebrania na ina maana ya kuchoka na kupiga miayo, Mke wa kwanza wa Yakobo kwenye Biblia. Yakobo alimpenda Raheli ambaye alikuwa mdogo wake na Lea kwa sababu Raheli alichangamka bali Lea aliuonekana na mchovu sawa na jina lake

Kelvin – Neno la kiskotish au kiingereza  likiwa na maana ya rafiki wa meli

Je wewe jina lako au la mtoto wako lina maana gani?

Leave your comment about Majina Maarufu Yenye Maana Mbaya using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here