Mama Wema Sepetu Atoa Msimamo Kuhusu Kurudi CCM

0
40

MAMA WEMA ATOA MSIMAMO HATIMA YAKE CHADEMA

Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting

MAMA WEMA ATOA MSIMAMO HATIMA YAKE CHADEMA

Mmama mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Miriam Sepetu amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na mwanae wana mpango wa kurudi katika chama cha Mapinduzi (CCM).
Februari 25 mwaka huu Wema na mama yake walijivua uanachama wa CCM na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kwenda kupigania demokrasia ya kweli.
Juzi katika mitandao ya kijamii jana, mama wema alieleza yeye na mwanae wataendelea kuwa wanachama wa Chadema na mwanaye.
“Mimi ninachoona CCM wana akili ya kutaka kuvuruga Chadema. Na tuwe makini kwa maeneo ya kutuvuruga kwa kipindi hiki tujenge chama.
“Kuna watu ambao si waelewa kabisa na CCM wanajua nguvu ya Wema na yangu zilivyo, waje wabomoe nyumba, ‘Notes’ wametoa lini ya kubomolea hii nyumba? Basi kifo cha wengi ni harusi.
“Mimi nitakuwa chadema pamoja na mwanangu na mimi ndiye msemaji mkuu. Wao waje wabomoe tu nipo teyari. Kwanza hawanibomoi mimi. Wanabomoa nyumba ya marehemu Sepetu,” alisema mama wema.
Wakati wakijiunga na chadema, walisema wamejiunga na chama kilichoisumbua CCM wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Naye wema alisema alijiunga Chadema bila kulipwa chochote na iwapo ikibainika kinyume kaburi la baba yake Zanzibar lipasuke katikati.

Leave your comment about Mama Wema Sepetu Atoa Msimamo Kuhusu Kurudi CCM using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here