Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Sayari ya Venus (ZUHURA)

1
914
Sayari ya Venus
 • Venus ni sayari ya pili katika mfumo wa jua.
 • Kwa kiswahili hujulikana kama zuhura
 • Ni sayari inayoongoza kwa kung’aa kuliko sayari zote angani.
 • Hujulikana kama morning star na evening star
 • Venusi ipo umbali wa km milioni 107 kutoka kwenye jua
 • Ni sayari pekee iliyo karibu na dunia
 • Venus iko umbali wa km milioni 38 kutoka sayari yetu ya dunia
 • Ni sayari inayo lingana na dunia katika umbo, saa nyingine Venus na Dunia huitwa sayari pacha

Sifa za kipekee ambazo huwezi kuzikuta kwenye sayari zingine ni

 1. Venusi hutumia siku 243 kujizungusha katika muhimil wake, maana yake siku moja ya Venus ni sawa na siku 243 za kidunia. 
 2. Venus hutumia siku 224 kumaliza mwaka mmoja kulizunguka jua, ina maanisha kwamba siku moja ya Venus ndefu kuliko mwaka.
 3. Sayari nying huzunguka kutoka kushoto kwenda kulia au kutoka magharibi mwa mhimili wake kwenda mashariki yaani clockwise lakini Venus kama ilivyo Uranus huzunguka kutoka kulia kwenda kushoto au kutoka mashariki kwenda magharibi mwa mhimili wake yaani anti-clockwise au kinyume chake, bado wanasayansi wa anga za juu hawaja pata sababu za hizi sayari mbili kuzunguka kinyume
 4. Venus ni sayari yenye joto kali sana linalofikia 470, yaani sayari ya mercury iliyo karibu na jua haina joto kali kama linalopatikana Venus. Hii ni kwa sababu Venus ina volcano nyingi kuliko sayari yeyote katika mfumo wa jua ,kuna aina 1600 za volcano katika safari ya venus. Kwa sababu ya volcano kila kona sayari ya Venus ina joto kali sana kuliko sayari zote hata ile ya Mercury (Zebaki)ambayo ndio iko karibu na Jua.
 5. Venus ina hewa ya ukaa (carbon dioxide) nyingi katika anga lake na kwa hiyo ni sayari yenye anga chafu kuliko sayari yeyote katika mfumo wa jua huku ikiwa imetawaliwa na gesi chafu ya carbon dioxide. Pia kutokana kuwa na anga chafu inakuwa ni vigumu sana kuifanyia uchunguzi sayari hii ambapo wana astronomia wanashindwa kuitazama sura yake vizuri kwakutumia telescope kutoka duniani.
 6. Venus haina mwezi hata mmoja unaoizunguka sayari hii.
 7. Ni sayari inayo ng’aa sana katika mfumo wa jua huwa inaonekana muda mfupi baada ya jua kuzama upande wa magaribi, huwa inaonekana katika nyuzi 45. Pia asubui inakuwa ya mwisho kupotea baada ya nyota zote kupotea na huwa ina ng’aa sana ndiyo maana ikaitwa ZUHURA. Ndio maana huitwa ZUHURA au Morning Star/Evening Star.
 8. Ukizipanga sayari zote nane katika sayari zinazoweza kusuport life basi venus itakuwa ya mwisho kutokana na kuwa na hewa nyingi sana ya ukaa yaani carbon dioxide na gesi zingine nyingi chafu pamoja na vimbunga vingi na volcano zinazolipuka muda wote.
 9. Umbile la ndani la Venus ni kama la dunia kwa hiyo ina Brittle layer kama ya Earth Crust, Ina MANTLE na METALLIC CORE ambazo ndizo sehemu muhimu ya Dunia.
 10. Pia inakisiwa kuwa miaka ya mwanzoni (kati ya bilioni 3 na miaka milioni 600 iliyopita) wa kuwepo kwa uhai duniani, anga la Venus ilikuwa ni kama la dunia kabla haijachafukwa na hewa ya ukaa kama ilivyo sasa na kwa hiyo inakisiwa pia kuwa kuna kila dalili kuwa kulikuiwa na uhai mdogo kwenye baadhi ya maeneo hapo zamani.

Kumbukumbu:

Urusi lilikuwa taifa la kwanza kutuma chombo kwenda sayari ya Venus miaka iyo ya 1970’s lakin vyombo vingi vilikuwa vikiungua kabla ata ya kufika lakin ata vyombo ambavyo vilifika vili tuma picha hafifu mda mfupi kabla ya kuungua kutokana na joto lililopo katika venus lakin miaka ya mbeleni urusi na Marekani walifanikiwa kufanya mission za kutuma vyombo katika sayari iliyo karibu na dunia kwa ajili ya kuichunguza Venusi.

Leave your comment about Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Sayari ya Venus (ZUHURA) using the comment form below

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here