Maoni zaidi kuhusu mgogoro wa Acacia Mining na serikali ya Tanzania

0
97

Acacia nasikia wamefungua kesi mahakama ya biashara ya kimataifa wakitaka makontena yakaguliwe na wakaguzi wasioegemea upande wowote, hiyo ni sawa ila serikali iwe makini hapo.

Lakini tusiandikie mate, kontena bado ziko na nafikiri chini ya ulinzi wa serikali. Zikaguliwe hata na neutral auditors ili tujue ni data zipi ziko sawa na nani kaibiwa au nani anaonewa.

Kwa hali iliyopo inaonyesha ACACIA na wawekezaji wao, yaani Barick Gold ya Canada hawako kwenye good terms na kwamba hao wawekezaji walitaka kuuza share zao kwa muda mrefu. Hii inaonekana wazi kwa sababu BarickGold hawataki kuwashiriksiah Acacia kwenye mazungumzo na serikali na wao Acacia wanadai matokeo ya mazungumzo isipowapendela wataenda mahakamani. 

Mwaka jana BarickGold almanusura wauze share zao zote kwa kampuni nyingine ya Kanada (Endeavour Mining) ila ilitibuliwa na katazo la Rais la kusafuirisha kontena nje. Kwa hali hii siwaamini Acacia kabisa na nadhani kuna uhujumu sio tu kwa serikali bali pia kwa huyo mwekezaji wao yaani BarickGold ya Kanada

Leave your comment about Maoni zaidi kuhusu mgogoro wa Acacia Mining na serikali ya Tanzania using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here