Mbowe, Slaa, Lissu Lema na wenzake watajwa na Zitto kuwa wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa za maji taka

0
1173
Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo Wakiongea na Vyombo vya Habari tarehe 24 Novemba 2013
Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo Wakiongea na Vyombo vya Habari tarehe 24 Novemba 2013
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe  amehitimisha kwa kudai kuwa yeye na wenzake yaani akina Dk Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na wa nne ambaye bado hajajulikana kuwa wao wanataka mabadiliko. Aliendelea kujitofautisha na wenzao ndani ya CHADEMA kuwa Mbowe, Slaa, Lissu Lema na wenzake watajwa kuwa wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa za maji taka kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hili hapa chini:

 

Akina Zito, Dr Kitila, Samson Mwigamba na mwingine wa nne

Mbowe, Dr Slaa, Godbless Lema, Tundu Lissu na wenzake

Wapenda demokrasiaWahafidhina
Waumini wa uwajibikajiWabadhirifu
Wapenda siasa safiWatukuzao siasa za majitaka.

 

Haya yamechukuliwa kwenye hitimisholake sehemu D kama ilivyonukuliwa hapa chini
d) Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni
mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa
uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa
majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi
shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata
kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, ‘kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika
nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo’, na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa
chama chetu.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013

Leave your comment about Mbowe, Slaa, Lissu Lema na wenzake watajwa na Zitto kuwa wahafidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa za maji taka using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here