Mbunge wa Bukoba (CHADEMA) Mh. Wilfred Lwakatare ni Mgonjwa

0
343
Mh. Wilfred Lwakatare ni Mgonjwa

KWA UFUPI
– Mbunge wa Bukoba Wilfred Lwakatare ni Mgonjwa
– Alilazwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa Hindu Mandal
– Mama Tibaijuka amefanya jitihada kubwa kuhakikisha Lwaka anapata matibabu sahihi
– CHADEMA hawataki taarifa za ugonjwa wake zijulikane kutokana na nafasi yake ndani ya chama
– Watoto wake wameambiwa wasitoe kwenye public taarifa za ugonjwa wake
– Mtoto wake wa kike ndiye anayerun social networks za baba yake kama facebook, whatsapp na Instagram

Mbunge wa Bukoba mjini Mh. Wilfred Lwakatare ni mgonjwa ambapo aliwahi kulazwa ICU Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hindu Mandal. Mama Tibaijuka alipomtembelea hospitalini Dodoma, ndipo wananchi tukajua kumbe Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA ni mgonjwa. Mama Tibaijuka na wabunge wengine wa mkoa wa Kagera walichanga fedha na kumkodia ndege binafsi ya kumpeleka Dar es Salaam ambako amelazwa kwenye hospitali ya Hindu Mandal ambapo alipelekwa moja kwa moja ICU. Inadaiwa kuwa Mheshimiwa Lwakatare yupo hoi sana kiasi cha kutokujitambua. Ugonjwa unaomsumbua bado ni siri ingawa taarifa nyingine zinadai kuwa kichwa kinamuuma sana.

Pamoja na hali hiyo, CHADEMA hawaguswi kabisa na ugonjwa wa Mkurugenzi wao wa Ulinzi na Usalama na kwamba hakuna kiongozi yeyote wala mwenye chama, Edward Lowasa aliyefika hospitalini kumjulia hali. Inaelezwa pia kuwa jitihada zinafanyika ili taarifa za Lwakatare ziwe siri. Na watu wake wa karibu wameambiwa wasiiongelee kwenye public hali ya Lwakatare hasa watoto wake wanaopenda kuandika mengi juu ya baba yao.

Mtoto wake wa kike aliyeacha kusoma Chuo cha Sokoine sababu anataka apelekwe nje ya nchi ndie yupo busy kumsaidia hospitali baba yake na kuendelea kutumia social netowrks za baba yake kama facebook, Instagram na whatsapp kurusha habari kama vile ni yeye mwenyewe, wakati hana nguvu kabisa.

Lwakatare ameanza kuumwa ugonjwa usiojulikana katika kipindi ambacho alikuwa anaendesha vuguvugu la chini kwa chini kwa kutumia Makachero wake kumshughulikia Lowasa ili asiwe mgombea wa CHADEMA 2020.

Yote kwa yote Lwakatare ni mgonjwa na wana Bukoba wanapaswa kujulishwa kuwa Mbunge wao ni Mgonjwa. Pamoja na kwamba nilipambana naye sana wakati wa ile VIDEO YA LWAKATARE kama ilivyorushwa na Bukoba Boy, hakika nimejawa na huruma sana kuugua kwake kwani hata mwaka hajamaliza kuwatumikia wana Bukoba.

Chanzo: Mwanahalisi Forum

Leave your comment about Mbunge wa Bukoba (CHADEMA) Mh. Wilfred Lwakatare ni Mgonjwa using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here