Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, “Ni lini mara ya mwisho umemwambia mumeo “Nakupenda”?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
- Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
- Wengine jana,
- Wengine wiki iliyopita
- Wengine mwezi uliopita
- Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno “NAKUPENDA MPENZI”
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Katika majibu hayo, meseji za vichekesho zilikuwa ni nyingi na kweli vichekesho vya ndoa ni nyingi kama ilivyosomwa katika hizo meseji, fuatilia hapa zaidi.
Simu ya 1 – “Samahani, nani mwenzangu”!
Simu ya 2 – “wrong number”!
Simu ya 3 – “samahani, umekosea namba”!
Simu ya 4 – “Si nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hii”!
Simu ya 5 – “Mh! leo mvua itanyesha”!
Simu ya 6 – “Nikija tutaongea zaidi”!
Simu ya 7 – “……Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ……”!
Simu ya 8 – “Me too”!
Simu ya 9 – “Huu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikoma”!