Meseji za Vichekesho

15
76315
meseji ya vichekesho

Jamaa mmoja alimuaga mke wake wa kuwa anakwenda safari kumbe huku nyuma kapanga kusafiri na kujirusha na bi . Baada ya kujirusha kwa usiku mmmoja kesho yake akiwa ofisini aliamu kumtumia meseji ya shukrani bi na meseji ilikuwa hivi:

“Asante mpenzi kwa staili uliyonifanyia jana usiku, umekosha moyo wangu sitasahau mpenzi. Na mimi nitakutunza leo, miss you”

Kwa bahati mbaya bila kukusudia aliweka namba ya bi mkubwa yaani waifu wake badala ya bi na alibofya kidude cha send. Meseji ilienda moja kwa moja kwa mke wake yaani waifu.
Jamaa kuona hivyo haraka akawahi ofisi za fokodam (kampuni ya simu) na kumuuliza karani kama anaweza kuzuia meseji isimfikie waifu wake.

Karani naye katoa mpya kwa kamuambia awahi kwenye mnara ili aweze kuzuia. Hata hivyo meseji hiyo ilimfikia waifu….

Leave your comment about Meseji za Vichekesho using the comment form below

15 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here