Misemo ya Hekima Kutoka kwa Wahenga

12
4661
 1.  “Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo.” *Napoleon_Bonaparte.*
 2. “Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake.” *George_Patton.*
 3. “Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa.” *John_Adams.*
 4. “Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi.” *Sun_Tzu.*
 5. “Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda.” *Harry_Browne.*
 6. “Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso.” *Adolf_Hitler.*
 7. “Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea.” *Friedrich_Nietzsche*
 8. “Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka.” *Confucus*
 9. “Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo.” *Albert_Einstein.*
 10. “Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote.” *Plato.*
 11. “Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo.” *Harry_Truman*
 12. “Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili.” *Benjamin_Franklin*
 13. “Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria” *Lamar_Smith*
 14. “Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa” *Doug_Larson*
 15. “Siasa ni hatari kuliko vita. Kwenye vita mtu hufa mara moja tu, lakini kwenye siasa mtu hufa na kufufuka mara nyingi kadri iwezekanavyo” *WinstonChurchil*

Leave your comment about Misemo ya Hekima Kutoka kwa Wahenga using the comment form below

12 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here