MKE WA DKT SLAA ATAKIWA MAHAKAMANI KESI YA LULU

0
53

Mahakama kuu ya Tanzania, yamtaka mke wa Dkt. Slaa kwaajili ya kutoa ushahidi katika kesi ya kuuwa bila kukusudia inayomkabili mwigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu).

Katika kesi hiyo, Josephinie Mshumbusi ni miongoni mwa mashahidi upande wa utetezi aliyetakiwa kutoa ushahidi wake leo au askari aliyechukua maelezo yake kutokana na kwa sasa kuishi nje ya nchi.

Mahakama Kuu ya Tanzania imelazimika kuahirisha kesi ya mauaji bila kukusudia inayomkabili msanii wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu hadi October 25, 2017 baada ya shahidi Josephine Mushumbus ambaye ni mke wa Katbu Mkuu wa zamani wa , Dr. Wilbroad Slaa kutofika Mahakamani.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea na ushahidi wa upande wa utetezi 'Lulu' leo mbele ya Jaji Sam Rumanyika.

Wakili wa Lulu, Peter Kibatala amemueleza Jaji Rumanyika kuwa wamefanya jitihada za kumpata Mushumbus lakini imeshindikana.

"Hivyo tunaiomba Mahakama tuwasilishe maelezo ya shahidi huyo Mushumbus ikiwezekana tuyasome hapa Mahakamani."

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Faraja George aliweka pingamizi akidai kuwa Kibatala hawezi kuvaa kofia mbili ya uwakili na ushahidi.

Kutokana na hatua hiyo, Jaji Rumanyika alitoa uamuzi na kuamuru kwamba kama Mushumbus hawezi kufika basi aliyemuandikia maelezo yake anapaswa kufika Mahakamani.

"Mtu wa muhimu ni aliyeandika maelezo ambaye ni Detective Sajent Nyangea ambaye anapaswa kuyasoma maelezo hayo."

Baada ya kueleza hayo, Jaji Rumanyika ameahirisha kesi hiyo hadi October 25, 2017.

Image may contain: 1 person, sitting and closeup

Image may contain: 2 people, people sitting

Leave your comment about MKE WA DKT SLAA ATAKIWA MAHAKAMANI KESI YA LULU using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here