Mohamed Ali Afariki Dunia Katika Umri wa Miaka 74

0
611
Muhammad Ali Afariki Dunia akiwa na miaka 74

Bingwa wa dunia kwa upande wa ngumi uzito wa juu kwa takriban miongo mitatu Muhammad Ali Afariki dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Muhammad Ali (Jina lake la awali kabla hajabadili dini ni Cassius Marcellus Clay, Jr.) alizaliwa tarehe 17 Januari 1942 na akafariki dunia Ijumaa ya tarehe 3 Juni 2016 ni sawa na takriban miaka 74. Alizaliwa katika mji wa Louisville, Kentucky, Marekani na akafariki katika mji wa Phoenix, Arizona, Marekani.

Tarehe April 28, 1967 Muhammad Ali aliwashangaza Wamarekani wengi baada ya kutangaza rasmi kuachana na Ukristo (Baptisti) na kujiunga na Uislamu (Black Muslims). Inasadikika alifanya mageuzi hayo ili kukwepa majukumu ya kwenda vitani Vietnam.

Amezaa watoto 9 ambao ni

  1. Laila Ali,
  2. Rasheda Ali,
  3. Hana Ali,
  4. Asaad Amin,
  5. Maryum Ali,
  6. Jamillah Ali,
  7. Khaliah Ali,
  8. Muhammad Ali Jr.,
  9. Miya Ali

Muhammad Ali alipigana kwenye masumbwi mara 61 na kushinda mara 56 zikiwemo knockout 37 na kufanya kuwa rekodi ya mara zote na hivyo kuitwa “The Greatest of all the time”. Alipigana na kushinda mfululizo mara 31 kabla hajapigwa na Fraizer  tarehe 8 Machi 1971

Pambano la kihistoria ambalo litakumbukwa na wengi ni lile lililokatiwa jina la “Rumble in the Jungle,” lililofanyika Zaire ambalo Ali alipambana na George Foreman akiwa na umri wa miaka 32 na kumtwanga kwa knockout -TKO. Ali aliutumia mfumo au staili ya “rope-a-dope” mfumo huu unajifanya umenaswa kwenye kamba halafu adui wako anajikuta akitupa ngumi nyingi zisizo na madhara ambazo mwisho wake zitamchosha na kum ruhusu Ali kupiga kirahisi kwa TKO

Don King; “It’s a sad day for life, man. I loved Muhammad Ali, he was my friend. Ali will never die,”

Don King, alishiriki kusimamia baadhi ya mapambano makubwa ya Ali

Muhammad Ali alikataa kwenda kushiriki vita vya Vietnam miaka ya 1960 kwa sababu za imani yake ya kiislam.

Ali alitupa ngumi 29,000 katika taaluma yake na kupata kipato cha dola milioni 57 ambazo hata hivyo hazikuweza kumuepusha na madhara ya ngumi hizo na ndio ikampelekea kupata ugonjwa wa Parkinson (Ugonjwa wa kutetemeka)

Pambano la tarehe 12 Octoba 1980 kati yake na Larry Holmes ndilo hasa linasadikiwa limeletea matatizo ya ubongo yaliyompelekea kutetemeka na hadi kumchukua mauti.

“If I had known Holmes was going to whip me and damage my brain, I would not have fought him,” Ali said. “But losing to Holmes and being sick are not important in God’s world.”

“Kama ningelijua holmes alikuwa anakwenda kunipiga na kuniharibu ubongo nisingepigana naye” ali alisema, “lakini kupoteza kwa holmes na kuwa mgonjwa sio muhimu katika ulimwengu wa watu wa mungu”

Kwa upande wake Muhammad Ali hakulaumu kwa ugonjwa alioupata kwa sababu ya ngumi badala yake alisema

“What I suffered physically was worth what I’ve accomplished in life,” he said in 1984. “A man who is not courageous enough to take risks will never accomplish anything in life.”

“ugonjwa niliyoupata ina dhamani sawa na mafanikio katika maisha yangu” alisema mwaka 1984.  “mtu ambaye sio jasiri kudhubutu hawezi kamwe kufanikisha jambo lolote maishani”

Mimi binafsi namkumbuka Mohamed Ali alipotembelea Africa alisema Waafrika wana sura nzuri kuliko wazungu. Alionyesha kwa dhati upendo wake kwa waafrika tofauti na superstar wenzake weusi kama akina marehemu Michael Jackson na wengine walio hai. Mfano Maiko Jackson alipotua Afrika alishika pua kuonyesha kuwa Africa inanuka.

Mohamedi Ali alikuwa na busara sana na hii inajitokeza kwenye malezi ya watoto wake hasa mmojawapo wa binti yake alivyoanza kuwa na tabia mbaya ya kuvaa vibaya alitumia hekima kumrudi kwa maneno ya hekima.

“I prayed to Allah to protect me from enemies, suddenly I began losing friends”

Muhammad Ali is a real Superstar and the Legend of the century

Leave your comment about Mohamed Ali Afariki Dunia Katika Umri wa Miaka 74 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here