Ndoa ya Morgan Tsvangirai na Elizabeth Macheka Yavunjika

0
2163
Zimbabwe Morgan Tsvangirai Wedding

Ndoa ya Kiongozi wa chama kikuu cha upinzania cha Zimbabwe, Ndugu Morgan Tsvangirai imevunjika na wamekuwa wakiishi mbali mbali kwa miezi sasa.

Ndoa ya Tsangirai na Elizabeth Macheka Yavunjika
Waziri mkuu wa Zimbabwe, Tsvangirai na mke wake mpya Elizabeth Macheka
Waziri mkuu wa Zimbabwe adai amempata penzi la kweli la moyo wake kwa Elizabeth Macheka

Waziri mkuu huyo wa zamanai wa Zimbabwe alimpoteza mke wake Suzan kwenye ajali ya gari mwaka 2009. Alimuoa haraka haraka Lorcadia Karimatsenga mwaka 2012 lakini ilimbidi amuache kwa gharama ya dola 200,000 za kimarekani ili aweze funga ndoa na  Macheka.

Tsangirai na Macheka wakifishana pete
Tsvangirai, 60, aliyevaa suti nyeusi na Elizabeth Macheka, 35, ndani ya gauni la harusi wakivishana pete huko Harare kwenye harusi iliyoshuhudiwa na mamia ya waalikwa. Rais Mugabe na baadhi ya viongozi wakubwa serikalini walioalikwa hawakuhuduria bila sababu kujulikana
Tsvangirai na Elizabeth Macheka wakibusiana
Tsvangirai, 60, aliyevaa suti nyeusi na Elizabeth Macheka, 35, ndani ya gauni la harusi wakibusiana huko Harare kwenye harusi iliyoshuhudiwa na mamia ya waalikwa. Rais Mugabe na baadhi ya viongozi wakubwa serikalini walioalikwa hawakuhuduria bila sababu kujulikana

Gazeti la The Herald limetaarifiwa kwa uhakika kuwa Ms Macheka alitoka nyumbani mwa Mr Tsvangirai mwezi uliopita alipokuwa Nigeria akikutana na nabii TB Joshua. Sasa Ms Macheka anaishi sehemu ya Philadelphia ya Borrowdale wakati ndugu Tsvangirai  akibakia huko nyanda za juu.

Vyanzo vyetu  vinadai kuwa ndugu wa karibu wa familia wamejaribu kusuluhisha ndoa hii bila mafanikio.

Baba yake na Elizabeth amejaribu kumshauri binti yake hata kwa kumtembelea huko Borrowdale lakini Elizabeth hakutoa ushirikiano.

Morgan Tsvangirai na Elizabeth Macheka
Waziri mkuu wa Zimbabwean, Morgan Tsvangirai mchumba wake Elizabeth Macheka katika mojawapo ya shughuli za uma

Akihojiwa na vyanzo vya habari hii ndugu Tsvangirai amethibitisha kuwa mke wake kahama huko ndani na hajui sababu hasa za kuhama

Akihojiwa kwenye simu baada ya nguvu na muda mwingi kutumika ili kumpata, Elizabeth hakutaka kusema lolote badala yake alidai

Hameno Tsvangirai ndiye anayejua zaidi. Wakati mke wake anahojiwa, Tsvangirai alikuwa mtu wa huzuni . “Nampenda sana mke wangu na nimefanya kazi ngumu sana kuitunza familia yangu” alisema

“Kama nijuavyo, bado niko kwenye ndoa na mke wangu na hakuna sababu ya kuzungumzia talaka hapa. Ndoa ni ya watu wawili waliodhamiria kupendana na kusaidiana na kuwa na furaha. Kama kuna tofauti, kitu ambacho sio ngeni, tutayajadili kama watu wawili wazima. Hayo ndio ninajituma nayo. Ndoa yetu ni ya uma na hivyo kufuatiliwa na watu ni kawaida lakini ukweli ni kwamba hakuna wazo la kutengana hapa ” Mr Tsvangirai alisema

Alikanusha taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wakuu wa MDC-T kuwa nyumba iliyoko Borrowdale anayoishi kwa sasa Elizabeth imejengwa kwa fedha za chama.

Leave your comment about Ndoa ya Morgan Tsvangirai na Elizabeth Macheka Yavunjika using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.