Home Blog Page 328

Je Wajua Juu ya Mgomo wa Madaktari Tena

0
mgomo wa madaktari tena

mgomo wa madaktari tenaTaarifa hapa chini imetolewa na chama cha madaktari Tanzania (MAT) na inaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mgomo kuanza tena baada ya tarehe 7 Machi 2012. Kwa undani zaidi endelea kusoma taarifa yenyewe:

05/03/2012
MSIMAMO JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI

KAMA  TULIVYOTOA  TAARIFA  KWENYE  KIKAO  CHA  MADAKTARI  CHA  MARCH
3,  NI  KWAMBA

MAKUBALIANO  YALIYOFIKIWA  NA  HATIMAYE  KUTIWA  SAINI  KATI  YA
SERIKALI  NA
MADAKTARI TAREHE 2/3/2012 NI KUWA, ILI MEZA YA MAZUNGUMZO YA KUJADILI
MADAI
YA MADAKTARI IWEZE KUENDELEA NA HATUA YA PILI NI LAZIMA WAZIRI WA AFYA
(DR MPONDA) NA NAIBU WAKE (DR LUCY NKYA) AMA WAJIUZULU AU WAWAJIBISHWE
KAMA

ILIVYOKUWA IMEAHIDIWA NA MH. WAZIRI MKUU FEBRUARY 9 ALIPOFANYA KIKAO
NA WATUMISHI WA AFYA PALE HOSPITALI YA MUHIMBILI.

AIDHA,  KULINGANA  NA  MAKUBALIANO  HAYA  KIKWAZO  KIKUBWA  CHA
KUTOKUENDELEA  KWA MAJADILIANO  YA  MADAI  YA  MADAKTARI  (UBORESHAJI
WA  HUDUMA  WAPATAZO  WAGONJWA,

MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYIA KAZI NA MASLAHI KWA UJUMLA WAKE) NI
KUENDELEA KUWEPO KWA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA KWENYE NAFASI ZAO ZA
KIUONGOZI.

HIVYO BASI, KWENYE HUO MKUTANO WA MARCH 3, BAADA YA MAJADILIANO NA
TAFAKARI ZA KINA, ILIKUBALIWA KWA PAMOJA KUWA WATU HAWA WAWILI
WANATAKIWA KUACHIA NGAZI   MARA   MOJA   ILI   HAKI   ZA   WAGONJWA
NA      MADAI   YA      MADAKTARI       YAWEZE KUJADILIWA NA KUTEKELEZWA.

HIVYO  BASI,  ILIAMULIWA  KUWA  KAMA  MPAKA  SIKU       YA  JUMATANO
(MARCH  7)  BADO AKINA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA WATAKUWA BADO WAPO
MADARAKANI      WATAANZA MGOMO  RASMI  KUSHINIKIZA  AMA  WAJIUZULU  AU
WAWAJIBISHWE  ILI  TARATIBU  ZINGINE ZIWEZE KUANZA.

KAMA ILIVYO TARATIBU YA CHAMA KUTOA TAARIFA KWA WANACHAMA KOTE NCHINI,
IFAHAMIKE KWAMBA MKUTANO ULIAMUA KUWA MADAKTARI WOTE KUWA KUANZIA
JUMATANO (MARCH 7)  WATASITISHA  KUTOA  HUDUMA  ZOTE  ZA  AFYA  KATIKA
HOSPITALI       ZOTE NCHINI     MPAKA HAPO SERIKALI  ITAKAPOONESHA  UTAYARI KWA
KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUWAWAJIBISHA    WATAJWA HAPO JUU ILI HATUA
ZINGINE ZA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI KWA        MANUFAA YA TAIFA
YAWEZE KUANZA KUSHUGHULIKIWA.

IFAHAMIKE   KWAMBA   CHAMA   KINASIKITISHWA   SANA   NA   KITENDO
CHA   VIONGOZI WAANDAMIZI  WA  WIZARA  YA  AFYA  AMBAO  WANAJUA
UMUHIMU  WA  KUWAJIBIKA.  KWA  MARA NYINGINE  TENA  WANAWAFANYA
MADAKTARI  WAENDELEE  KUTETEA  HAKI  ZA  WATANZANIA

KATIKA NJIA NGUMU NA KWA NIA YA KUFANIKISHA MALENGO HAYA KWA FAIDA YA
WATANZANIA WOTE.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAT MAKAO MAKUU.

DR. NAMALA MKOPI RAIS WA MAT

MARCH  7

Taarifa ya Kuuawa kwa Dr Harison Mwakyembe

1
Dr Harrison Mwakyembe

Dr Harrison MwakyembeTaarifa ya kuuawa kwa Dr Harison Mwakyembe na Wenzake iliandikwa na Mwakyembe mwenyewe miezi sita kabla hajapewa sumu na kuiwasilisha Polisi.

Tuhuma za kutaka kuuawa kwa Dk.Mwakyembe na wenzake kwa IGP, Februari 8, mwaka jana, Dk. Mwakyembe alizungumza na baadhi ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi makao makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam, na kuelezea wasiwasi wa kuuawa kwake. Dk. Mwakyembe katika barua yake, aliyotakiwa kuliandikia jeshi la Polisi, kwenye barua hiyo, ilinukuliwa hivi;

Na Harrison Mwakyembe

“Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakyembe iliendelea kueleza;“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hiibila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea Januari 22, 2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa Januari 21, 2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 68… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 68…).

Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T7…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.

“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”; Mkusa,jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa;na mtu mwingine (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.

“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya (kaitaja) akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina (linahifadhiwa). Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kurogwa” safari hii.

Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Willbrod), Anne Kilango Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mark Mwandosya na Benard Membe.

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.

“Usiku wa Jumamosi Januari 22, 2011 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo, (kwa gari aina ya Defender STK 26…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve With Impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea Januari 29, 2011 na kesho yake Januari 30, 2011 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T7… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo).

Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T8… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: Februari 5, 2011, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili: moja ya polisi (PT 02…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Ushiriki wa Al Shabaab;

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al- Mujahideen (kwa kifupi Al- Shabaab). “Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini.

Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini la Uislamu kutishiwa.

Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu. “Niliweza vilevile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao.

Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo. “Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Februari, 2009).

Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa: “(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi Februari 5, 2011 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile ‘portion’ ya mganga ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni); “(b) Kesho yake (Jumapili) Februari 6, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T3… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).

“Waliomo kwenye kikosi hicho ni Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye Januari 19, 2011 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T6…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.

“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji. “Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili.

Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi: “Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T8… AQS) Januari 8, 2011 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa polisi Morogoro. “Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life.

Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli ya….(jina la hoteli na mmiliki tunalo). “Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T8… AQS, VX Land Cruiser STK 1…, Mercedes Benz (Station Wagon) T8… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T2… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T6… APF, Nissan Patrol T8… ADH.”

“Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata vyanzo vyangu vya habari ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.

“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani iko siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake wasitake, hakika ni suala la muda tu. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa taifa letu, taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.

“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia Kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji”, mwisho wa waraka wa Dk.Harrison Mwakyembe kwa jeshi la Polisi.

Mauaji Haya ya Songea Hayakubaliki

0
mauaji ya kikatili songea
mauaji ya kikatili songea
mauaji ya kikatili songea
Waendesha pikipiki (Bodaboda) Wakiandamana Kupinga Mauaji ya kikatili Songea

Waendesha pikipiki songea wakiwa wamefunga barabara inayoelekea kwa mkuu wa mkoa ili kushinikiza serikali kuzuia mauaji ya kikatili ya raia zaidi ya 15 wasikuwa na hatia wanaoendelea kuuwa Songea na watu wasiojulikana tangu mwezi novemba mwaka jana 2011.

 

 

 

Jaribio la kutorosha Mali Nje Lazimwa

0

Je wajua kwamba Rostam Aziz ajivua gamba CCM

 

 

Baada ya kujivua gamba, sasa Rostam Aziz ataka kujivua uraia wa Tanzania kwa kutorokea Indonesia.. Jaribio la kutorosha mali zake nje lazimwa. Nadhani sasa anajionyesha kuwa hakuwa mwenzetu. baada ya kupora mali za nchi na baada ya Dowans kulipwa sasa nataka kuhamisha utahiri wake wote Indonesia ambako nahisi ndiko asili yake.

By: Lilian Kivuyo

Ufisadi wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya -Blandina Nyoni Huu Hapa

0
Ufisadi wa aliyekuwa Katibu Mkuu WIzara ya Afya Huu Hapa

Ufisadi wa aliyekuwa Katibu Mkuu WIzara ya Afya Huu HapaYafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-

 1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
 2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.
 3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.
 4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.
 5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict ofInterest’
 6.  Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema ninikuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni EliasMkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damudamu na ni afisa ugavi wa wizara
 7. Amemkopesha gari la serikali ainaya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahilikukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali,anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguumitatu (Bajaj)
 8. Amenunua vingamuzi vya magari manne kwa shilingi 1.3Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single sourceprocurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzihaya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Internsdoctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa namadeni lukuko.
 9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamishakiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwendaNational Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazinakwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAGkatika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010
 10. Mwishoni mwamwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bilakibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo piazilihojiwa na CAG.
 11.  Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wadunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifawa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zotezilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi nikwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspentbalances.
 12.  Amekuwa akizua uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda),Chief Internal Auditor (Bi Anna J Mhere) na Director of Administration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katikautendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant marambili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administrationand Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wawakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubalichochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikalimfano katika maeneo ya Manunuzi.
 13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu waKitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe kwa kukataakununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihojini kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba nahawajashindanishwa.
 14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili naUtalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadiWizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa ummaambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama nadereva au / na secretary
 15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkyakutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informerwake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo.Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.
 16. Akiwa Wizara ya Maliasili naUtalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawahawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo
 17.  Yeye ndiye chanzo chamasahibu yanayowakabili Watanzania hivi leo kwa kukosa huduma ya afyakwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwakuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali

Je Wajua Mamilionea wa Kike Afrika

0
Charnley Irene

Haya ni maneno yangu, wanawake watachukua nafasi kubwa ya kiuchumi Afrika katika karne ya 21. Fuatilia orodha hii hapa chini jinsi wanawake wanavyoendelea kuwa mamilionea wa karne ya 21

Isabel Dos Santos (Angola)Isabel Dos Santos (Angola)

Jina: Isabel Dos Santos
Raia: Angola
Net Worth: Unknown
Chanzo: Uwekezaji
binti wa kwanza wa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, Isabel dos Santos alianza biashara katika umri wa miaka 24 kwa kutumia ushawishi wa baba yake kupata faida kubwa ya mikataba. Anaendelea na mahusiano ya karibu na Ureno. Kento Holding ni kampuni ya Maltese yenye usajili  ambayo yeye ni mmiliki na ana hisa 10% katika Zon Multimedia, kampuni ya Kireno ya conglomerate. Yeye alipewa hisa ya Euro milioni 164 mwaka 2010. Pia anamiliki hisa kubwa katika benki za Kireno ambazo ni Banco Espirito Santo na Banco Português de Investimento, na katika Energias de Ureno, ambayo inazalisha na kusambaza umeme.

 

Bridgette Radebe (Afrika Kusini)Bridgette Radebe (Afrika Kusini)

Jina: Bridgette Radebe
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: Unknown
Chanzo: Madini

Dada mkubwa wa bilionea wa Afrika Kusini, Patrice Motsepe, Bridgette Radebe alianza kama mwendesha mikataba ya kuchimba madini miaka ya 80s, kusimamia shafts na kununua nyumba kubwa za madini. Alianzisha kampuni ya madini Mmakau Mining, na kupata mafanikio makubwa ya madini katika platinum, dhahabu makaa ya mawe, uranium,, chrome, utafutaji na maslahi ya madini. Pia hutumika kama rais wa Jumuiya ya Madini Afrika Kusini. Aliolewa na Jaji wa Afrika Kusini Waziri, Jeff Radebe.

 

 

 

 

 

 

 

 

Irene Charnley (Afrika Kusini)

Charnley Irene

Jina:  Irene Charnley
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R234.4 milioni / $ 34,726,511 USD
Chanzo: MTN

Kiongozi wa zamani wa vyama vya wafanyakazi alikuwa kama nguzo muhimu katika mpatanishi wa Umoja wa Kitaifa wa Mineworkers nchini Afrika Kusini. Mkurugenzi Mtendaji katika MTN, kampuni ya mawasiliano kubwa zaidi katika Afrika, ambapo yeye aliongoza kampuni kwa mafanikio ya kuingiza katika nchi kadhaa za Afrika. Alikuwa mtu muhimu katika mazungumzo kwa ajili ya kupata na moja ya leseni nne za GSM katika Nigeria. Yeye pia amesaidia MTN kupata leseni ya pili GSM katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa upande wake, alipata zawadi kubwa ya hisa MTN yenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 150 mwaka 2007 katika mazingira ya kutatanisha. Sasa ni mtumishi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Smile Telekom, kampuni ya simu za gharama nafuu nchini Mauritius.

Pam Golding (Afrika Kusini)Pam Golding (Afrika Kusini)
Jina: Pam Golding
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R637, 525,000,000 / $ 94,447,247 USD
Chanzo: Real Estate

Mmoja wa kingunge anayejulikana sana Afrika Kusini katika biashara ya ardhi na majumba, Alianzisha Pam Mali Golding mwaka 1976 bila mtaji wowote na msaidizi. Kampuni yake kwa sasa ni moja ya  makampuni makubwa Afrika Kusini yanayofanya biashara za ardhi na majumba. Mwaka 2010 mauzo yalifikia dola za kimarekani 1,700,000,000 sawa na randi bilioni 11.  Ameshastaafu ussimamizi wa kazi lakini bado mwenyekiti. Kwa sasa anajitolea zaidi kwenye kazi za kijamii.

 

 

 

 

 

 

 

Wendy Appelbaum (Afrika Kusini)
Jina: Wendy Appelbaum
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R1.233 bilioni / $ 182,713,341 USD
Chanzo: Bima

Binti wa pekee wa bilionea wa zamani wa Afrika Kusini, Donald Gordon, Wendy alikuwa mkurugenzi katika Liberty Investors, kampuni ya zamani ya Liberty Group – ilihusika zaidi na mambo ya bima na ardhi na majumba. Aliuza hisa zake zote na kubaki na utajiri wa pesa. Pamoja na mume, Hylton Appelbaum, walinunua DeMorgenzon. Walichangia pia dola za Marekani 23,000,000 (R150 milioni) ili kujenga Gordon Institute of Business Science (Gibs), na Donald Gordon Medical Center. Wendy ni mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Afrika Kusini wa Professional golfers

Elisabeth Le Roux Bradley (Afrika Kusini)

Jina: Elisabeth Bradley
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R1.754 bilioni / $ 259,927,377 USD
Chanzo: Uwekezaji

Baba wa Elisabeth Bradley, Albert Wessels alileta Toyota (TM) Afrika Kusini mwaka 1961. Mwaka 2008, Wesco Investement ya  Afrika Kusini wanaomiliki kampuni ambayo yeye udhibiti, aliuza hisa zake 25% katika Toyota Afrika Kusini kwa Toyota Motor Corp nchini Japan kwa dola za Marekani $ 320,000,000 sawa na R2.1 bilioni. Aliondoka pale na angalau dola za Marekani $ 150,000,000 sawa na R1 bilioni. Bradley ina mjumbe katika bodi ya makampuni ya bluu Chip kama vile Benki ya Standard Bank Group, Hilton Hotel na Roseback Inn..

Wendy Appelbaum (South Africa)Mamphela Ramphele (Afrika Kusini)
Jina: Mamphela Ramphele
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R93 milioni / $ 13,805,316 USD
Chanzo: Uwekezaji

Mkurugenzi wa mara moja wa Benki ya Dunia na sasa anaongoza Ventures Capital Circle, Taasisi inayoongoza kwa kuwezehsa weusi kiuchumi. Daktari na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi wa zamani ambaye  pia ni moja ya vingunge maarufu wa Afrika. Aliwahi kuwa mkurugenzi katika Anglo-American, Remgro na Mediclinic. Pia yupo katika Bodi ya Wadhamini ya Rockefeller Foundation, Mo Ibrahim Foundation na Umoja wa Mapinduzi ya Kijani Afrika.
Elisabeth Le Roux Bradley (South Africa)Sharon Wapnick (Afrika Kusini)
Jina: Sharon Wapnick
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R161.76 milioni / $ 23,974,938 USD
Chanzo: Real Estate, huduma za fedha

Mmoja wa wanahisa wakubwa zaidi katika Octodec Investments and Premium Properties, makampuni yote mbili zimeorodheshwa katika soko la hisa la Afrika Kusini. Makampuni hayo yalianzishwa na Baba yake, Alec Wapnick. Anafanya kazi kama mkurugenzi asiye mtendaji katika Octodec, na ni mshirika katika Attorneys, taasisi ya sheria yenye mafanikio makubwa Johannesburg.
 

 

 

 

 

 

 

Wendy Ackerman (Afrika Kusini)Wendy Wendy Ackerman (Afrika Kusini)

Jina: Wendy Ackerman
Raia: Afrika Kusini
Net Worth: R3.37 bilioni / $ 500,552,252 USD
Chanzo: Biashara rejareja

Pamoja na mume wake, Raymond, yeye anamiliki Family Ackerman Trust ambayo kwa karibu 50% ya Pay Pick ‘n’, moja ya maduka rejareja ya Kusin ambalo ni kubwa zaidi katika Afrika. dola za kimarekani 3 bilioni, kampuni inafanya kazi pia nchini Namibia, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe na Australia. Wendy anafanya kazi kama mkurugenzi mtendaji wa kikundi. Sanaa connoisseur ni mdhamini wa Cape Town Opera Trust.