Paul Pogba Asaini Mkataba wa Kufuru na Manchester United

0
125
Uhamisho wa Paul Pogba Kufuru

Paul Pogba center forward wa Juventus mabingwa wa Italia amesiani mkataba wa miaka mitano (5) na Machester United kwa uhamisho wa paundi milioni 89 na kufanya kuwa ni uhamisho wa dhamani na wa historia katika ligi ya Uingereza katika msimu huu wa kiangazi.

Uhamisho huu utafanya kuwa wa gharama kupita uhamisho wowote katika ulimwengu wa soka duniani. Pamoja na kuwa haijadhihirishwa bado lakini fununu zinasema kuwa klabu ya Juventus itabeba kitita cha paundi milioni 140 hivi kwa ajili ya uhamisho huu na kuipita ile rekodi iliyowekwa na Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspur kwenda Real Mardid ya Hispania.

Yeye atakuwa akilipwa Paundi laki 3 (300,000) kwa wiki kwa muda wa miaka mitano (5)

“Ni mchezaji machachari sana” Jose Mourinho alisema hayo jumapili baada ya timu yake kuifunga mabingwa wa Uingereza wa mwaka 2015/16 Leicester City kwa mabao 2:1. “Kama mambo yote yakienda vyema, tumempata mchezaji muhimu sana na pia tuna timu nzuri”

https://youtu.be/ou96MRwQXfs

Paul Pogba alikuwa ni mchezaji katika timu ya academy ya Machester United ambamo alijiunga mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 16 lakini mwaka 2012 alitoka huku akichanganyikiwa kwa vile hakupewa nafasi katika timu kama mchezaji wa kwanza hivyo akaamua kuhamia Juventus ambamo ndiko alikopatia mafanikio yote haya. Katika muda wote akiwa Juventus Pogba amekuwa ni mchezaji nyota katika safu ya kiungo na ushambuliaji. Akiwa Juventus, Pogba amkiwezesha kikosi hicho kutwaa mataji manne na kukiwezesha pia kufika fainali ya UEFA ya mwaka 2015.

Leave your comment about Paul Pogba Asaini Mkataba wa Kufuru na Manchester United using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here