Kwa maneno mafupi tu, Raheem Sterling amefunga mabao ambayo yameipaisha Man City kuwa point 15 juu ya wengine wanaofukuzia kombe la EPL. Kwa maneno mengine goli moja lenye pointi 3 muhimu ni bora kuliko magoli mengi yasiyo na point. Pale City wanapokuwa na uhaba wa magoli, Sterling anatokea na kufunga bao. Mfano mzuri ni lile la Man city na New Castle.
Kwa upande mwingine, Harry Kane pamoja na nyota yake ya Kufunga magoli kuwa nzuri mwaka huu pengine kuliko miaka mingine lakini timu yake ni ya ya sita (6) katika mzunguko wa 22 wa ligi ya Uingereza wakati Mancity ya Sterling inaongoza kwa pointi 15. Pia Mohamed Salah pamoja na kuvunja rekodi ya Suarez katika kufunga magoli mengi akiwa na klabu ya Liverpool, bado liverpool ni ya nne (4) katika mzunguko wa 22 wa ligi.
Msimamo wa Ligi ya Uingereza katika mzunguko wa 21 ni kama ilivyoonyeshwa hapa chini: