Rais wa Tanzania Mhe. DK. John Magufuli Awateua Wakuu wa Mikoa

0
689
Mhe. Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
 • 13 ni wapya
 • 12 waachwa
 • 7 wabakizwa
 • 5 wahamishwa
 • 1 apangiwa mkoa mpya wa Songwe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. DK. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa 26 ya Tanzania Bara ambapo kati yao 13 ni wapya, 12 wameachwa, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Akitangaza uteuzi huo tarehe 13 Machi 2016 Ikulu Jijini Dar esalaam, Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe alisema kuwa wakuu wa Mikoa walioteuliwa wataapishwa siku ya jumanne ya tarehe 15 Machi 2016 saa tatu na nusu Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Wakuu wa mikoa ni kama ifuatavyo na mikoa yao kulia:

 1. Mhe. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
 2. Mhe. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
 3. Mhe. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
 4. Mhe. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
 5. Mhe. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
 6. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
 7. Mhe. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
 8. Mhe. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
 9. Mhe. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
 10. Mhe. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
 11. Mhe. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
 12. Mhe. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
 13. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zelote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
 14. Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
 15. Mhe. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
 16. Mhe. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
 17. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
 18. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
 19. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 20. Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
 21. Mhe. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
 22. Mhe. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
 23. Mhe. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
 24. Mhe. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
 25. Mhe. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
 26. Mhe. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

 

Leave your comment about Rais wa Tanzania Mhe. DK. John Magufuli Awateua Wakuu wa Mikoa using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here