Tanzania Serengeti Boys Yaifunga Angola AFCON U17 2017

0
28
Timu ya Taifa la Tanzania ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 inayoshiriki mashindano ya kombe la Afrika (AFCON U17 2017) huko nchini Gabon imepata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Angola. Wakicheza kwa kujiamini zaidi na kushambulia kwa kasi, Serengeti Boys waliweza kupata ushindi wa magoli mawili dhidi ya moja la Angola.Kasi ya kushambulia iliweza kuzaa matunda katika dakiaka ya sita pale Kelvin Nashin Naftal alipotumbukiza goli safi la kichwa kwenye wavu wa vijana wa Angola.Hata hivyo vijana wa Angola walijitutumua na kusawazisha katika dakiak ya 17 kwa goli lililofungwa na Pedro. Mpaka wanaenda mapumziko magoli yalikuwa ni 1:1.
Serengeti Boys baada ya kusikiliza mawaidha ya viongozi wao katika kipindi cha mapumziko, walirudi na ari mpya na kucheza mpira wa kutulia na wa malengo na hivyo katika dakika ya 68 Abdul Hamis Suleiman alitumia vyema nafasi iliyotokana na uzembe wa mabeki wa Angola kupachika goli la pili na la ushindi kwa Vijana hao wa Serengeti.Tanzania waliweza kulilinda lango lao kwa uimara zaidi na hivyo kutowaruhusu Angola kupenyeza kwenye eneo la hatari na mpaka mwisho ubao ulisomeka hivi:  
Tanzania 2: 1 Angola
Katika mchezo wa kwanza Serengeti Boys iliweza kutoka sare na mabingwa watetezi wa kombe hilo Mali kwa bila ya kufungana.
Kwa sasa Serenegti Boys wamefiksiha alama 4 na magoli mawili dhidi ya moja la kufungwa na hivyo kufungana kwenye nafasi ya kwanza na Mali ambazo zote zina alama 4, magoli mbili ya kufunga na goli moja la kufungwa. Kundi B lina timu za Mali, Niger, Angola na Tanzania.
Baada ya Mali kuwafunga Niger goli 2:1 sasa Tanzaia itahitajika sare tu kwenye mechi yake dhidi ya Niger ili kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia kule India. Afrika itawakilishwa na timu nne (4) zitakazoingia nusu fainali ya AFCON huko Gabo Mei 2017.Timu zinazoshiriki ziko nane kama ifuatavyo:

Kundi A: Gabon, Ghana, Guinea, Cameroon
Kundi B: Mali, Angola, Niger, Tanzania
Kila kundi litatoa timu mbili na Tanzania ikitoa sare mchezo wake na Niger itakuwa alama 5 ambayo inaweza kufikiwa na Mali tu

Leave your comment about Tanzania Serengeti Boys Yaifunga Angola AFCON U17 2017 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here