Sheria ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji Kwenye Katiba Mpya

0
197

18(1)Kiongozi wa umma hatashiriki katika kufanya uamuzi wa jambo au shughuli yoyote ambayo ana maslahi nayo yeye binafsi,mwenza wake,mtoto wake,jamaa yake,rafiki au mtu yeyote wa karibu.(2)Kiongozi wa umma hatazungumzia kitu chochote katika Baraza la Mawaziri,Bunge,Kamati au chombo kingine chochote rasmi ambacho ana maslahi nacho ya moja kwa moja au vinginevyo,isipokuwa tu kama atatoa taarifa ya mgongano huo wa maslahi katika chombo hicho.(3)Itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi wa umma kushiriki katika uamuzi unaohusu kuongeza au kuboresha maslahi kwa namna yoyote ile yanayohusu wadhifa alionao,na endapo atashiriki,basi masharti hayo mapya yataanza kutumika kwa kiongozi wa umma atakayekuja baada ya kiongozi husika kuondoka au kumaliza muda wa kukaa katika nafasi ya madaraka iliyompatia fursa ya kushiriki katika kuamua maslahi husika.(4)Masharti ya ibara ndogo ya (3)hayatamhusu kiongozi wa umma ambaye kutokana na asili ya nafasi ya madaraka au aina ya kazi zake anapaswa kushiriki katika upangaji wa mishahara au maslahi mengine ya watumishi wa umma.

(b)hauhatarishi maslahi ya umma kwa ajili ya maslahi binafsi;au(c)haushushi hadhi ya ofisi anayofanyia kazi.(2)Kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (1)mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kusimamia utekelezaji wa masharti yanayohusu kanuni za uongozi wa umma.(3)Wadhifa wa”Kiongozi wa umma” kama ulivyotumika katika Sehemu hii utajumuisha viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa kama watakavyoainishwa kwenye sheria za nchi. 15.-(1)Kiongozi wa umma wakati anapotekeleza shughuli za kiserikali,akipewa zawadi,zawadi hiyo itakuwa ni mali ya Jamhuri ya Muungano na ataiwasilisha kwa Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara au kiongozi wa taasisi ya Serikali inayohusika, akiainisha:(a)aina ya zawadi;(b)thamani ya zawadi;c)sababu ya kupewa zawadi; na(d)mtu au mamlaka iliyotoa zawadi hiyo.(2)Neno “zawadi” kama lilivyotumika katika Ibara hii linajumuisha kitu chochote chenye thamani atakachopewa Kiongozi wa umma katika utekelezaji wa shughuli za umma.

(5)Kiongozi wa umma hataruhusiwa kushika nafasi za madaraka zaidi ya moja au kutumikia Mihimili ya Dola zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja.19.Kiongozi wa umma hataruhusiwa kutumia au kuruhusu kutumika kwa mali yoyote ya umma,zikiwemo zilizokodishwa kwa Serikali,kwa madhumuni ya kujipatia yeye binafsi au kumpatia mtu mwingine manufaa yoyote.20(1)Bunge litatunga sheria itakayosimamia,pamoja na mambo mengine:(a)utaratibu wa utwaaji wa mali za viongozi wa umma zilizopatikana kwa kukiuka sheria;(b)utaratibu wa kumwajibisha Kiongozi wa umma aliyekiuka maadili na Miiko ya Uongozi;na(c)uanzishaji wa mitaala inayohusu Katiba,maadili na uraia,shuleni na vyuoni.(2)Masharti yaliyoainishwa katika Sehemu hii ya Sura ya Tatu yatatumika pia kwa watumishi wa umma baada ya kufanyiwa marekebisho stahiki.

(3)Bunge litatunga sheria itakayosimamia,pamoja na mambo mengine,thamani,kiwango,aina na uhifadhi wa zawadi kwa Jamhuri ya Muungano. 16. Kiongozi wa umma -(a)hatafungua au kumiliki akaunti ya benki nje ya Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kwa namna ambayo sheria za nchi zinaruhusu; na(b)hataomba au kupokea mkopo au faida yoyote kwa namna au mazingira ambayo yanashusha hadhi au heshima ya utumishi wa umma.17(1)Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha,ndani ya siku thelathini baada ya kupata uongozi na baada ya kuacha uongozi, mali na thamani yake na madeni yake katika Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.(2)Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1),Kiongozi wa umma atalazimika kutangaza na kuwasilisha taarifa ya mali na madeni:(a)yake binafsi;(b)ya mwenza wake wa ndoa; na c)ya watoto wake walio chini ya umri wa miaka kumi na nane, mara moja kila mwaka kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji.3)Bunge litatunga sheria itakayosimamia,pamoja na mambo mengine:(a)ngazi au orodha ya viongozi wa umma wanaopaswa kutangaza mali na madeni yao; na(b)utaratibu wa kuwasilisha taarifa ya mali na madeni kwa Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji kwa mujibu wa Katiba hii.

 

Leave your comment about Sheria ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji Kwenye Katiba Mpya using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here