SIASA NI VITA ISIYO MWAGA DAMU NA HAINA RAFIKI WALA ADUI WA KUDUMU!

0
461
Edward Loawassa Akikaribishwa rasmi CHADEMA

Ujio wa Edward Lowassa kwenye a UKAWA kumeibua maneno mengi na sintofahamu kwa watu mbali mbali wakiwemo wana baadhi ya na wana UKAWA. Ipo mitazamo tofauti. Kuna wanaoona Lowassa asingepokelewa na UKAWA. Wengine wanaona Lowassa angepokelewa lakini asingepewa jukumu la kupeperusha bendera ya kugombea urais kupitia na UKAWA. Na wengine wana sema imejimaliza kabisa kwa kumpokea Lowassa.

Maoni ya wengi wanaoona Lowassa asingepokelewa UKAWA na yanajikita kwenye historia ya ndugu Lowassa, kwamba alikuwa ambayo imekumbatia ufisadi na Lowassa akiwa mtuhumiwa wa ufisadi hasa wa kashfa ya Richmond na alitajwa kwenye orodha ya aibu pale Mwembeyanga. Ni sahihi kabisa kwamba alituhumiwa, na ametoka iliyochafuka. Lakini, kuja kwake UKAWA kunaweza kuwa ni chanya kwa ujumla wake na dalili zinaanza kuonekana. Hivyo ninawaomba tutafakari pamoja katika makala hii.

Wakati vita ni siasa inayomwaga damu, wachina wana msemo unaosema siasa ni vita isiyomwaga damu. Hivyo, jambo la kwanza kukubaliana hapa ni kwamba siasa ni vita. Chanzo cha vita ni nini ? chanzo cha vita kimo ndani ya mioyo yetu ambapo mawazo mabaya, mawazo ya ubinafsi na mawazo ya kutimiza tamaa zetu hutoka. Vita inaanza na tofauti ya mawazo na baadae mitazamo na shabaha au malengo. Abdul Baha aliwahi kusema, chanzo cha vita vinavyotokea hapa duniani ni uchoyo na ukatili wa binadamu, chanzo cha yote haya ni tamaa ya maendeleo ya kimwili ambayo kilele chake ni maisha ya anasa. Katika hali hii ndipo wakubwa wanapojikuta wapo tayari kuwaonea wanyonge na kuwa tayari hata kuwanyang’anya kile kidogo walicho nacho. Na wanyonge wanapokataa kuachilia vile vidogo walivyo navyo, wakubwa hawa huwa tayari kuwaua huku wakitoa kisingizio hiki na kile. Na ndipo vita hutokea. Jamii zilizotofautiana kimawazo, mtazamo na baadae shabaha hupingana na kuanza kupigana kwa kutumia silaha na hatimae kumwaga damu na hata kupoteza maisha. Na ndiyo maana wahenga walisema mtu aliyejasiri ni yule ambaye anayeweza kuutawala moyo wake na hivyo basi jemedari jasiri na hodari hapigani vita. Siasa ni vita isiyo mwaga damu. Jamii inaweza kutofautiana kimalengo, kishabaha lakini hupingana kwa hoja bila kuchukua silaha, hivyo hawamwagi damu au kupoteza maisha.

Moja ya kanuni ya vita ni kwamba, kama jirani yako ni adui wa adui yako basi huyo shirikiana nae huyu ni rafiki yako kwani atakusaidia kufikia malengo yako. Na kama jirani yako ni rafiki wa adui yako, basi uwe makini nae kwani huyo ni adui yako, kwani atashirikiana na adui wako kukuzuia kufikia malengo yako.
Kanuni nyingine mhimu ni kwamba, katika vita mambo hubadilika kila wakati na hivyo husababisha mikakati, mbinu na michakato ya kufikia malengo kubadilika pia. Mfano, adui yako akibadilisha silaha na wewe itabidi ubadili silaha. Au jiografia ikibadilika na wewe kama jemedari itabidi ubadili mbinu. Lakini kwenye vita pia huwa kuna propaganda zenye lengo la kumpumbaza au kumtia hofu adui au kumchanganya. Yote hayo yanahitaji kubadili mbinu au mikakati kwa kasi ili kufikia malengo yako.

Ukichukua kanuni ya kwanza na ya pili maana yake ni kwamba hakuna adui wala rafiki wa kudumu katika vita. Hivyo basi, kama siasa ni vita isiyomwaga damu, vilevile kwenye siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu.

Baada ya maelezo hayo, nieleze kidogo kuhusu Lowassa. Lowassa alikuwa ni mwana aliyekubalika mpaka chama kikamwamini na kumpa dhamana ya kuwa Waziri Mkuu katika serikali yake. Lowassa amepata tuhuma akiwa ambayo kisiasa alikuwa na ni adui wa . Katika siasa Lowassa alikuwa ni adui wa . Hili liko wazi. Lowassa ameamua kujitoa , amekuwa ni adui wa . Kulingana na kanuni za vita, adui wa adui yako itabidi ushirikiane nae kwani atakusaidia kufikia malengo yako. Malengo ya UKAWA ni kuchukua dola, hivyo UKAWA walipomfuata Lowassa ili wafikie malengo ya kuchukua dola ni jambo sahihi. Huyu alikuwa adui wa UKAWA kabla jina halijakatwa, lakini inabidi awe rafiki baada ya kuhama . Adui wa ni rafiki wa UKAWA.
Niwakumbushe kuhusu sakata la Lembeli huko Kahama. Wakati Lembeli anahama CCM alieleza mara nyingi mambo aliyotendewa na uongozi wa Mkoa wa Shinyanga ukiongozwa na Khamisi Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga. Mgeja alikuwa adui wa Lembeli. Lembeli ameondoka CCM na amekuja Chadema. Baada ya wiki kadhaa, Mgeja nae amekuwa ni adui wa CCM, amekihama na amejiunga na Chademaamepokelewa. Lembeli na Mgeja inabidi washirikiane kuiondoa CCM madarakani huko Kahama na Shinyanga, kwani adui wao ni mmoja hivyo ni marafiki kwa kanuni za kivita. Walikuwa ni maadui, dynamics zimebadilika wanakuwa ni marafiki. Lakini pia tunakumbuka sana Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dare s salaam alivyokuwa akiishambulia sana Chadema. Kwa sasa ni adui wa CCM na hivyo ataisaidia Chadema kupata ushindi.
Mwaka 1995, Dk Slaa alishinda kura za maoni huko jimbo la Karatu kupitia CCM lakini jina lake lilikaktwa. Dk Slaa alihamia Chadema zikiwa zimebaki siku mbili tu ili kampeni zianze. Chadema ilimpokea na akapewa dhamana ya kupeperusha bendera kugombea ubunge kupitia Chadema. Dk Slaa kabla ya kujiunga na Chadema alikuwa CCM ambayo ni adui wa Chadema. Siku mbili baadae alikuwa ni adui wa Chadema na hivyo akawa rafiki wa Chadema. Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu. Na Kwa maoni yangu, ujio wa Lowassa kwenye UKAWA kama wana UKAWA watautazama hivyo itakuwa ni rahisi kushirikiana nae ili kuiondoa CCM madarakani.

Jambo jingine ambalo ninaona nilitolee maoni ni suala la dhamira. Nianze kwa kutumia mfano kutoka kwenye kitabu kiitwcho The Moral of the story. Kitabu hicho kinaeleza jinsi magazeti ya Marekani yalivyoripoti tukio moja la ajali ya moto iliyotokea kaskazini ya pwani ya magharibi ya nchi ile. Kwa mujibu wa kitabu hicho, “familia moja ilikwenda likizo fupi na kuacha funguo za nyumba kwa jirani ili amwagilie maji maua yao. Jumapili moja, saa kadhaa kabla ya familia hiyo kurudi, baridi ilikuwa kali. Jirani akaonelea ingekuwa vema awaandalie wenye nyumba makazi mazuri yenye joto. Hivyo, bwana yule aliingia ndani ya nyumba na kuwasha moto wa kuni kwenye tanuru. Kumbe, upepo wa mchana uliopita dirishani ulisababisha moto kusambaa ndani na kuteketeza nyumba. Wenye nyumba waliporudi walikuta majivu ya nyumba yao na kila kitu kikiwa kimetekea. Jirani huyu alikumbwa na huzuni kubwa baada ya magazeti kuandika kuwa alisababisha moto ule kwa makusudi.” Jirani aliyewasha moto, alilazimishwa kujibu maswali yaliyohusiana na hatma ama matokeo ya kitendo alichofanya. Hakuna aliyetafuta kujua ni kwa nini mtu huyu aliwasha moto ule, ili afahamu dhamira ya tendo lenyewe. Simulizi hii yatufundisha kwamba binadamu tunapaswa kuwahukumu wenzetu kutokana na dhamira zao na si kwa matokeo ya matendo yao peke yake.

Ujio wa Lowassa UKAWA umesababisha Dk Slaa kukaa kando kwa muda na Pofesa Lipumba kujiondoa kwenye nafasi ya uwenyekiti wa CUF. Wapo wana Chadema na wana CUF wanaowalaumu na kuwahukumu viongozi wa UKAWA kwa haya yaliyotokea. Lakini kulingana na simulizi ya The Moral of the story, binadamu tunapaswa kuwahukumu wenzetu kutokana na dhamira zao na si kwa matokeo ya matendo yao peke yake. Viongozi walioshiriki kumshawishi Lowassa kuja UKAWA wamesema waliona pasipo shaka kwamba Lowassa ataisaidia UKAWA kuiondoa CCM madarakani. Unaweza kusema dhamira ya viongozi hawa wa UKAWA ilikuwa kupata ushindi na kushika dola kwa kushirikiana na Lowassa. Dhamira hiyo ni njema. Hivyo tuwahukumu viongozi wa UKAWA kwa kuzingatia dhamira hiyo na wala si kwa kuondoka kwa Lipumba au kukaa kando kwa Dk Slaa. Na tukumbuke kwamba Lowassa hakuomba kujiunga na UKAWA bali UKAWA ndio waliomfuata na kumshawishi ahamie UKAWA na hatmae akakubali kubadilika ili kwa pamoja na UKAWA wayatafute mabadiliko ya watanzania nje ya CCM. Viongozi wa UKAWA hawatakiwi kuhukumiwa.
Ni muhimu kutambua kwamba wakati mwingine tuwe tayari kujitolea kufanya mambo au kuchukua maamuzi ambayo yataleta mafanikio, si kwetu sisi tu kwa wakati huu, bali yatalete mafanikio baadaye kwa faida ya watu wengine. Watu wanaoweza kufanya hivyo ndio watakaoleta mabadiliko yanayopasa, watu wa aina hiyo ni wachache sana duniani. Kwa mtazamo wangu viongozi wa UKAWA wanastahili kupongezwa kwa uamuzi wa kumshawishi Lowassa kujiunga na UKAWA. Watanzania wana kiu ya mabadiliko na wanaona watayapata nje ya CCM.

Pia niwakumbushe watanzania aliyowahi kusema Mwalimu Nyerere mwaka 1962 katika kitabu cha Tujisahihishe aliandika “Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo. Haujali adui wala rafiki, kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kuilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa nafikiri kuwa ni dogo au mpira natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani, ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa” Ni ukweli ulio dhahiri kwamba hakuna adua wala rafiki wa kudumu kwenye siasa na pia binadamu tunapaswa kuwahukumu wenzetu kutokana na dhamira zao na si kwa matokeo ya matendo yao peke yake.

Aidha niwakumbushe watanzania kwamba Mtu anayedhulumiwa haki yake kwa muda mrefu, licha ya kulalamika sana kisha akagundua kuwa hakuna mtu ambaye yuko tayari kumsikliza, basi atageuka kuwa mnyama. Anafikia hatua ya kutoona hata faida ya maisha yake. Hii ndiyo hulka ya binaadamu, awe mweupe au mweusi, wote wamezaliwa hivyo. Maisha ni matamu sana ndiyo maana hata mzee mwenye miaka 100 anapenda aishi angalau mwaka mmoja zaidi. Lakini maisha ni matamu na yenye thamani kubwa pale mtu anapopata haki yake, anapothaminiwa na kuheshimiwa. Watanzania wanataka mabadiliko yatakayowawezesha kuthaminiwa na kuheshimiwa katika matumizi ya rasilimali ya nchi yao.

Mwandishi wa Makala hii ni Fred Mpendazoe anapatikana kwa namba ya simu 0762 926 556 au 0787 638 575 au email fmpendazoe@hotmail.com

https://www..com/fred.mpendazoe.7/posts/135786593429443

Leave your comment about SIASA NI VITA ISIYO MWAGA DAMU NA HAINA RAFIKI WALA ADUI WA KUDUMU! using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.