Mwenyekiti wa Tumeya uchaguzi Zanzibar Salim Jecha Salim ametangaza kufuta uchaguzi wote wa Zanzibar wa Tarehe 25 Octoba 2015 pamoja na matokeo yake yote
Sababu kuu ni hizi hapa chini:
- Wajumbe wa tume kutofautiana na kupigana
- Wajumbe kuwa mashabiki wa vyama vya siasa badala ya kuwa kusimamia maadili ya tume
- Matokeo hasa ya Pemba kuwa na kura nyingi zaidi kuliko daftari la wapiga kura
- Kutolewa nje mawakala wa vyama vingine
- Kuvamiwa kwa vituo vya kupigia kura
- Vyama siasa kuingilia majukumu ya tume hasa kwa tukio la mgombea wa CUF, Maalim
- Seif kujitangazia ushindi kabla ya matokeo na mshindi kutangazwa na mwenyekiti wa tume
- Kuwepo kwa malalamiko mengi kuashiria kutoridhika na zoezi zima la uchaguzi
- Nambari za fomu katika karatasi za pemba kufutwa futwa