Ufisadi wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya -Blandina Nyoni Huu Hapa

0
1518
Ufisadi wa aliyekuwa Katibu Mkuu WIzara ya Afya Huu Hapa

Ufisadi wa aliyekuwa Katibu Mkuu WIzara ya Afya Huu HapaYafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-

 1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
 2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.
 3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.
 4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.
 5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict ofInterest’
 6.  Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema ninikuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni EliasMkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damudamu na ni afisa ugavi wa wizara
 7. Amemkopesha gari la serikali ainaya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahilikukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali,anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguumitatu (Bajaj)
 8. Amenunua vingamuzi vya magari manne kwa shilingi 1.3Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single sourceprocurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzihaya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Internsdoctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa namadeni lukuko.
 9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamishakiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwendaNational Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazinakwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAGkatika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010
 10. Mwishoni mwamwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bilakibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo piazilihojiwa na CAG.
 11.  Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wadunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifawa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zotezilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi nikwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspentbalances.
 12.  Amekuwa akizua uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda),Chief Internal Auditor (Bi Anna J Mhere) na Director of Administration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katikautendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant marambili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administrationand Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wawakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubalichochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikalimfano katika maeneo ya Manunuzi.
 13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu waKitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe kwa kukataakununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihojini kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba nahawajashindanishwa.
 14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili naUtalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadiWizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa ummaambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama nadereva au / na secretary
 15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkyakutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informerwake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo.Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.
 16. Akiwa Wizara ya Maliasili naUtalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawahawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo
 17.  Yeye ndiye chanzo chamasahibu yanayowakabili Watanzania hivi leo kwa kukosa huduma ya afyakwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwakuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali

Leave your comment about Ufisadi wa Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya -Blandina Nyoni Huu Hapa using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.