Ureno Mabingwa Wapya wa UEFA Euro 2016

0
305
Eder wa Ureno Akishuhudia Goli Euri2016

Mechi katika takwimu

  • Dakika; 120 (Fulltime)
  • Uwanja; Stade de France
  • Magoli; Ureno 1: Ufaransa 0
  • Mashuti golini; Ureno 9: Ufaransa 18
  • Mashuti yaliyolenga goli; Ureno 3: Ufaransa 7
  • Kadi za njano; Ureno 4: Ufaransa 6
  • Faulu; Ureno 12: Ufaransa 13

Timu ya taifa la Ureno imeweza kunyakua ubingwa wa Euro 2016 baada ya kuibwaga timu ya Taifa ya Ufaranza (Wenyeji) kwa goli moja lililofungwa na Eder aliyefunga kwa shuti kali upande wa kulia mwa golkipa wa Ufaranza katika dakia za nyongeza baada ya timu hizo kutoka bila ya kufungana katika muda wa kawaida.

Ushindi huu ni zaidi ya ushindi wa Taifa la Ureno, ni ushindi wa Christian Ronaldo dhidi ya wahasimu wake wakubwa hasa Lionel Messi wa Argentina.

Christian Ronaldo wa Ureno na Paul Pogba wa Ufaransa Katika Fainali za Euro 2016Ronaldo alidhiakiwa sana mwanzoni mwa mashindano haya waliomdhiaki wakisema kuwa hana mchango mkubwa katika timu yake ya Ureno kwenye mashindano makubwa kama haya. Hii inakuja sambamba na ukweli kuwa timu ya Ureno ilikuwa ni moaj ya timu ya kawaida kwenye mashindano haya ukiacha timu kama za Ubelgiji, Ujerumani, Whale na hata wenyeji wao Ufaransa. Ureno walianza kuonyesha umaridadi wao katika mechi ya Nusu fainali walipocheza na Whale kwa kuwafunga mabao 2 bila goli la kwanza likiwa la Ronaldo na lile la pili alilofunga Nani likiwa na shuti kali iliyopigwa na Ronaldo kuelekea golini kabla Nani hajaikatiza mwelekeo na kufanya goli la pili.

Katika mchezo wa leo Ufaransa ilitawala mpira kwa takribani 53% dhidi ya ile ya wenzao ya 47%. Ufaransa walipeleka mashambulizi mengi golini mwa Ureno isingekuwa umaridadi wa golkipa wa Uren leo hii Ureno ingelala kwa mabao sio chini ya 7. Ufaransa walipiga mashuti golini 18 dhidi ya 7 yaliolenga goli wakati wao Ureno walipiga mashuti 9 dhidi ya 3 yaliolenga goli na moja likazaa goli la ushindi  an ubingwa.

Hata hivyo Christian Ronaldo alifanyiwa changamoto ambayo mimi niliona kama faulu na Payet katika dakika ya 9 ya mchezo na hata baada ya kutibiwa na kurudi uwanjani hakuweza kuendelea na mechi na nafasi yake ikachukuliwa na Quaresma katika dakika ya 25. Ronaldo alitoka huku akibubujikwa na machozi ya huzuni kukosa mechi muhimu kama hii tena kwenye dakika za mwanzo. Kwa kawaida Ronaldo ambaye anaishezea Real Madrid ya Uhispania kama mshambuliajiu huwa anacheza mpaka mwisho hata zikiongezwa dakaika 30 yeye yumo hachoki. Kutoka kwa Ronaldo ni sawa na timu kupungukiwa mchezaji mmoja na hivyo iliiunua ari ya vijana wa kireno wakacheza kufa na kupona kuzua mashambulizi ya wachezaji mahiri kama akina Griezmann, Giroud, Pogba, Sissoko.

Kinachodhibitisha kwamba huu ulikuwa ushindi wa Ronaldo dhidi ya wahasimu wake ni hili, baada ya kupata matibabu Ronaldo alirudi kwenye benchi la wachezaji wa akiba ambako baada ya dakika za kawaida kuisha Ronaldo hakuweza tena kukaa kwenye benchi badala yake alikuwa sambamba na Kocha mkuu akihaha kuwahimiza wenzake wacheze vizuri. Pamoja na kuchechemea Ronaldo hakujali aliendea kukim,bia huku na huko akiwahimiza wenzake kushambulia.

Hatimaye katika dakika ya 109, Eder aliwakimbia mabeki wa Ufaransa na akiwa nje kidogo ya eneo la hatari aliachiua shuti kali lililompita kipa Lloris kwa upande wake wa kulia. Ronaldo atokwa tena na machozi safari hii yakiwa ni machozi ya furaha. Ronaldo sasa ndio hata hasikii tena kama anaumwa kwani alikuwa akihaha yeye na Kocha mkuu wakiwahimiza wenzake kulinda goli ambalo kweli Ureno waliweza kulinda hadi dakika ya 122 wakati ambao Refa wa mchezo alipuliza kipenga kuashiria kumalizika kwa mchezo.

Kutokana na ushindi huu sasa Ronadlo ameudhihirishia Ulimwengu na Wahasimu wake kuwa yeye ni bora kuliko Lionel Messi ambaye alishiondwa kuiletea Timu yake ya Taifa la Argentina kikombe chochote

 

Leave your comment about Ureno Mabingwa Wapya wa UEFA Euro 2016 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here