Utapeli Katika Ajira

0
1134

Wasiwasi wa kutokea kwa utapeli

Wiki iliyopita nilipigiwa simu na jamaa anayedai kunifahamu na kunisihi niwe mwakilishi wake hapa Arusha kwa ajili ya ajira ya wafanyakazi wa shirika lao linaloitwa APAPO. Alidai shirika limesajiliwa katika nchi nyingi Afrika lakini yeye ni mwakilishi wa Tanzania na makao makuu yapo Nzega

Hawakuwa wazi kwenye mambo mengi kama za ufunguzi wa ofisi na mikataba nk lakini provisionally niliwakubalia.

Waliponitumia Tangazo la kazi ghafla logic yangu ikaanza kuwa na maswali mengi na kurecall utapeli mbalimbali watu wanaotumia. Na mojawapo ya recal ni kuwa matapeli daima lazima wataje pesa. Kwenye tangazo kuna malipo ya kuomba kazi. DUH nikaona huu ni wizi wa mchana

Nikawaandikia hii email

Hello  Kapeele Sichula

 Thank you for the job vacancies document received correctly. I would only asked you one request

 Please remove my name and any contacts of me in the adverts until we have a formal agreement about this matter. My self am very keen on issues relating collecting cash from the public. Unless I understand well your operating policy and regulations plus any legal implications.

 These questions need to be clear to me before accepting the representation offer

1.    Staff recruitment without offices establishment

2.    Representative without formal agreement

3.    Recruitment with application fee without any governing state regulations or certification through TRA etc

4.    Too many staffs at the start without any other documentations and preparations

Lemburis Paul Kivuyo

 Wasiwasi wetu kuwa hawa ni matapeli

 Ajira wanazozitangazia ni Nyingi bila kuwepo kwa ofisi na taarifa zozote za ofisi na mpango wa kazi

 1. Ajira ya kada nyingi bila ya kuwepo bayana kazi watakazozifanya
 2. Ada ya maombi ya kazi
 3. Shirika kuenea Afrika kwa kasi katika uchanga wake
 4. Nembo yao kufanana na zile za mashirika ya umoja wa mataifa
 5. Mtandao wa facebook wa mhusika kuwa na marafiki wachache mno
 6. Sifa za waombaji kuwa rahisi. Yaani kuanzia darasa la saba
 7. Lengo la shirika liko pana mno na haijielezi kwa uwazi na undani zaidi
 8. Email ya info@apapoafrica.org na tovuti ya wwwapapoafrica.org haipo hewani

Madhara ya huu utapeli nukitokea

Maajenti wote walioorodheshwa hapo chini ninaamini hawajui huu utapeli na hivyo kuwa waadhirika baadaye jamaa wakifunga akaunti na kutokomea

Hatua nilizozichukua

1. Kuripoti polisi

2. Kuleta katika jukwaa hili ili kusambaza taarifa

3. Baadaye pia (kama siku tatu zijazo kuwatumia email wahusika waliotajwa kwenye listi

Tangazo la Kazi hili hapa (kiambatanisho kwa ajili ya original document)

UNITED AFRICANS

SHIRIKA LA UMOJA WA WAAFRIKA (APAPO)

        MIKOA YA RUKWA, KATAVI, KIGOMA, TABORA, SHINYANGA, KAGERA, LINDI, MBEYA, MOROGORO, ARUSHA, MWANZA NA DAR ES SALAAM.

 

APAPO ni kifupisho cha African Poor And Patient Organization. Ni shirika lililoanzishwa barani AFRIKA kwa sheria  Na. 24 ya mwaka 2002 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, (Reg. No. 00005441) lenye lengo la kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za jamii kwa wananchi hususani waishio maisha ya chini.

Kwa sasa shirika linatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

1. AINA YA KAZI: UWAKILISHI (Nafasi 12 kila Kijiji au Mtaa, Kata,                         

Tarafa, Wilaya na Mkoa.)

SIFA PEKEE

 • Mwombaji awe na Elimu ya darasa la saba au zaidi, Kujua kusoma na Kuandika.

 WAJIBU

Kuhamasisha na kuelimisha jamii, kusimamia na kutoa Haki, Misaada kwa wanachama na wahitaji wenye vigezo, kuwashauri viongozi wa dini na serikali, Kutatua migogoro kati ya shirika na wanachama, Kusajili Wanachama, Kuhakikisha Usalama wa wanachama na wasio wanachama katika maeneo yao kwa kushirikiana na Jeshi Polisi, Kubuni, Kusimamia na Kuendesha miradi ya Maendeleo ya shirika, kupokea, kujadili, Kuomba na Kupokea fedha au misaada toka mamlaka za juu au wahisani na kupitisha ama kurekebisha bajeti na Matumizi.

2. AINA YA KAZI: UKARANI (Nafasi 2 kila Kijiji au Mtaa, Kata,                         

Tarafa, Wilaya na Mkoa.)

SIFA PEKEE

 • Mwombaji awe na Elimu ya kidato cha nne (IV) au zaidi na Ujuzi wa Kutumia Kompyuta.

WAJIBU:     Kusimamia mgao wa fedha, Kufuatilia au Kukusanya ada za viingilio, uanachama, maombi ya kazi na kumkabidhi Mtunza hazina, Kuandika barua za safari za wanachama, wajumbe au watumishi.

 

3. MTUNZA HAZINA (Nafasi 1 kila Kijiji au Mtaa, Kata,                         

Tarafa, Wilaya na Mkoa.)

SIFA PEKEE

 • Mwombaji awe na Elimu ya kidato cha nne (IV) au zaidi na Taaluma ya uhasibu aliyoipata katika chuo kinachotambulikana na serikali.

 

WAJIBU:    Kupokea, Kupeleka au Kutoa fedha benki, Kuandika Hundi na Stakabadhi za malipo, Kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi, Kulipa mikopo, posho au mishahara na shughuli nyingine inayohusiana.

 

4. MAKATIBU WAHTASI-SECRETARIES (Nafasi 12 kila Mkoa)

 

SIFA PEKEE

 • Mwombaji awe amepitia mafunzo ya Ukatibu (Secretarial Course)

GRADE 1-111 katika chuo kinachotambulikana na serikali.

WAJIBU:     Kupokea simu na kuandika ujumbe, Kupokea na kuwaelekeza wageni, Kuchapa barua, Vyeti, Kutoa nakala za nyaraka mbalimbali, Kuandika muhtasari, Matangazo, Taarifa, Kutunza kumbukumbu katika majarada, Kuangalia matumizi ya Vifaa vitumiavyo umeme na kazi zingine zinazohusiana.

 

AFISA USALAMA (SECURITY OFFICERS) (Nafasi  8 Ofisi za Wilaya na Mkoa)

 

SIFA PEKEE

 • Mwombaji awe amepitia mafunzo ya jeshi.
 • Kwa  mstaafu(Polisi, JW,JKT na Magereza) awe amestaafu kati mwaka 2010-2013.

WAJIBU:     Kulinda Usalama wa wanachama, wawakilishi, watumishi, wananchi na mali zao, kusindikiza maofisa waandamizi na shughuli zingine zinazohusiana.

 

WANASHERIA (ADVOCATES, MEDIATORS AND ARBITRATORS) Nafasi 7 kila Mkoa.

 

SIFA PEKEE

 • Awe na shahada ya sheria.

WAJIBU:     Kusimamia wajibu na haki za shirika, wawakilishi, watumishi, wanachama  na wananchi kwa ujumla.

 

SIFA ZA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

Waombaji wawe tayari kuwa wanachama wa shirika ili kupata huduma muhimu za shirika,  akili timamu, Umri wa miaka 18 au zaidi, Moyo safi, Uadilifu, Uaminifu, Uvumilivu, Subira na Uwezo wa kufanya kazi mahali popote ndani na nje ya nchi.

 

UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI

(A) Ada isiyorudishwa ya kuomba nafasi ilipwe Katika Benki ya NMBTawi lolote nchini Tanzania A/C.  NO. 51110002370.

1. Ngazi ya Kijiji au Mtaa USD 10 au         T.shs 17,000/=

2.   Ngazi ya Kata USD 20 au                       T.shs 34,000/=

3.   Ngazi ya Tarafa USD 30 au                    T.shs 50,000/=

4.   Ngazi ya Wilaya USD 50 au                   T.shs 80,000/=

5.   Ngazi ya Mkoa USD 100 au                   T.shs 160,000/=

(B)  Barua za maombi ziambatane na nakala za Fomu za kuweka pesa benki (Pay in slip,) vyeti vyote vya Elimu, Ujuzi, Cheti cha Kuzaliwa, au Hati ya Kiapo (AFFIDAVIT) na picha mbili ndogo (Passport size.)

(C)  Waombaji wa Mikoani maombi yao yatapokelewa na wawakilishi wetu

 

RUKWA – LEONARD MICHAEL POULTIER P.O. BOX 36 SUMBAWANGA, SIMU: 0762 653439.

 

GEITA –  YOHANA KIDULA, SHULE YA MSINGI NYANKUMBU, P.O. BOX 27 GEITA SIMU; 0764497984

 

KATAVI – HAMIDA S. MBOGO, CCM MKOA, P.O. BOX 30, MPANDA SIMU: 0754 421318

 

KAGERA- SYLIVIA JOVIN, P.O. BOX 202 BUKOBA, SIMU: 0767 169313.

 

LINDI- WENSESLAUS MBILANGO P.O.BOX 328 LINDI, SIMU. 0787613615

 

SHINYANGA- EZEKIEL KAHONCA, P.O. BOX 470 SHINYANGA, SIMU: 0756 674528/0713 558118.

 

MBEYA- MWL. ZENITHA BAGAMOYO, P.O. BOX 1728, ITETE SHULE YA MSINGI –MBEYA. SIMU: 0753 281489.

 

MOROGORO- VENANCE MLALLY, CCM MKOA BUILDING LEFT WING 1ST FLOOR, P.O. BOX 6075, MOROGORO.

SIMU: +255 232600362/ 0754310762.

 

ARUSHA- LEMBURIS P. KIVUYO, P.O BOX 13143 ARUSHA. SIMU: +255 73 2978002/+255 787665050/+255 755646470.

 

MWANZA- EMIL ELIAS, INTERNET CAFÉ LUMUMBA STREET,

P.O. BOX 7774,MWANZA. SIMU:+255(0)282542569/ 0759707610.

 

DAR ES SALAAM- FREZA BWALYA, SUKARI HOUSE, 2ND FLOOR, SOKOINE/OHIO STREET, P.O. BOX 4825 DAR ES SALAAM. SIMU: 071219195940.

 

KIGOMA- JUMA SINGSON P.O. BOX 1196 KIGOMA SIMU: 0758 773285/0764918170, MAKOTI KASUJA, P.O. BOX 670 KIGOMA, SIMU: 0764110162.

 

KWA MAWASILIANO ZAIDI: KATIBU MTENDAJI, KANDA YA AFRIKA MASHARIKI, P.O. BOX 128 NZEGA-TANZANIA (EAZO)

SIMU: +255 262692406/0755844350

E-MAIL: achichief@rocketmail.com/info@apapoafrica.org

TOVUTI: WWW. envaya. Org/apapo

 

 MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI TAREHE 31/01/2013

Leave your comment about Utapeli Katika Ajira using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here