Utapeli kupitia mitandao kupitia namba 0783784005

0
946
Leo nilipokea simu kutoka namba hii hapa 0783784005 ikinitaka nijiunge na Freemason. Baada ya kukataa mpigaji alidai nisubiri mabaya yatakayonipata usiku wa Leo. Sauti yenyewe ilikuwa artificial. Yaani kama ya kijana wa kiume mdogo wa teenage hivi, halafu alikuwa akijitahidi kuongea sauti kwa kubadilisha (acting).
Baada ya kukata kama dakika mbili akapiga tena safari hii akitaka kusema jambo mara ikakatika aidha salio liliisha au betri iliisha chaji.
Watanzania sasa umaskini unawafanya kubuni miradi ya kitapeli ya kuwapatia riziki. Nafikiri kwa saikolojia yangu ndogo iliniambia huyu  kijana alikuwa akielekea kunipa option ya kufanya ili hayo mabaya yasinipate baada ya kunitishia.
Aidha nimtumie pesa au anything. Labda wenzangu mlishapatwa na utapeli huu mtanisaidia kwa faida yangu na wengine ambao hawajakutana na utapeli huu
Kama kawaida niliwapigia Airtel kuripoti hiyo namba na waliahidi kuifanyia kazi

Leave your comment about Utapeli kupitia mitandao kupitia namba 0783784005 using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here