Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba

0
201
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Watangazwa

KWA VYOMBO VYA HABARI

KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA MAALUM LA

UTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa la Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya , Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa la . Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.

2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika.

3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-

(i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20)
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

4. Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
5. Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

6. Kufuatia mwaliko huo, taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao. Mapendekezo hayo yalijumuisha majina 2,762 kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar mapendekezo hayo yalihusisha watu874. Hivyo basi, taasisi na makundi mbalimbali yalipendekeza jumla ya majina 3,636. Lakini, na kinyume na Sheria, watu 118 walijipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754.

7. Mchanganuo wa idadi ya watu walipendekezwa katika makundi mbalimbali ni kama ifuatavyo:

Na.Kundi/TaasisiTaasisi zilizoleta mapendekezoIdadi ya Watu WaliopendekezwaIdadi ya Wajumbe WanaotakiwaIdadi ya Walioteuliwa
TanzaniaBaraZanzibarTanzaniaBaraZanzibarTanzaniaBaraZanzibar
1.Taasisi zisizokuwa za Kiserikali246981,20344420137
2.Taasisi za Kidini55173448520137
3.Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu211412969422814
4.Taasisi za Elimu99844620137
5.Makundi ya Walemavu246974320137
6.Vyama vya Wafanyakazi201891319136
7.Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji814341073
8.Vyama vinavyowakilisha Wavuvi7345121073
9.Vyama vya Wakulima2281154420137
10.Makundi yenye Malengo Yanayofanana1422161311420146
Mapendekezo Binafsi118
Jumla6721782,88087420113467
Jumla Kuu8503,754

8. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopunguatheluthi moja wanatakiwa kutokaZanzibar na theluthi mbili kutokaTanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
9. Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.

WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA
10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijanawatu wazimana wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:

 

TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Magdalena Rwebangira2. Kingunge Ngombale Mwiru
3. Asha D. Mtwangi4. Maria Sarungi Tsehai
5. Paul Kimiti6. Valerie N. Msoka
7. Fortunate Moses Kabeja8. Sixtus Raphael Mapunda
9. Elizabeth Maro Minde10. Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda12. Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Idrissa Kitwana Mustafa2. Siti Abbas Ali
3. Abdalla Abass Omar4. Salama Aboud Talib
5. Juma Bakari Alawi6. Salma Hamoud Said
7. Adila Hilali Vuai
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Tamrina Manzi2. Olive Damian Luwena
3. Shamim Khan4. Mchg. Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora8. Hamisi Ally Togwa
9. Askofu Amos J. Muhagachi10. Easter Msambazi
11. Mussa Yusuf Kundecha12. Respa Adam Miguma
13. Prof. Costa Ricky Mahalu
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo2. Suzana Peter Kunambi
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu4. Fatma Mohammed Hassan
5. Louis Majaliwa6. Yasmin Yusufali E. H alloo
7. Thuwein Issa Thuwein
VYAMA VYOTE VYA SIASA
VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42)
TANZANIA BARA (28)
1. Hashim Rungwe Spunda2. Thomas Magnus Mgoli
3. Rashid Hashim Mtuta4. Shamsa Mwangunga
5. Yusuf S. Manyanga6. Christopher Mtikila
7. Bertha Ng’angompata8. Suzan Marwa
9. Dominick Abraham Lyamchai10. Mbwana Salum Kibanda
11. Peter Kuga Mziray12. Isaac Manjoba Cheyo
13. Dr. Emmanuel John Makaidi14. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
15. Modesta Kizito Ponera16. Prof. Abdallah Safari
17. Salumu Seleman Ally18. James Kabalo Mapalala
19. Mary Oswald Mpangala20. Mwaka Lameck Mgimwa
21. Nancy S. Mrikaria22. Nakazael Lukio Tenga
23. Fahmi Nasoro Dovutwa24. Costantine Benjamini Akitanda
25. Mary Moses Daudi26. Magdalena Likwina
27. John Dustan Lifa Chipaka28. Rashid Mohamed Ligania Rai
TANZANIA ZANZIBAR (14)
1. Ally Omar Juma2. Vuai Ali Vuai
3. Mwanaidi Othman Twahir4. Jamila Abeid Saleh
5. Mwanamrisho Juma Ahmed6. Juma Hamis Faki
7. Tatu Mabrouk Haji8. Fat –Hiya Zahran Salum
9. Hussein Juma10. Zeudi Mvano Abdullahi
11. Juma Ally Khatibu12. Haji Ambar Khamis
13. Khadija Abdallah Ahmed14. Rashid Yussuf Mchenga
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA
1. Dr. Suzan Kolimba2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo
3. Dr. Natujwa Mvungi4. Prof. Romuald Haule
5. Dr. Domitila A.R. Bashemera6. Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa
7. Prof. Bernadeta Kilian8. Teddy Ladislaus Patrick
9. Dr. Francis Michael10. Prof. Remmy J. Assey
11. Dr. Tulia Ackson12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu
13. Hamza Mustafa Njozi
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Makame Omar Makame2. Fatma Hamid Saleh
3. Dr. Aley Soud Nassor4. Layla Ali Salum
5. Dkt. Mwinyi Talib Haji6. Zeyana Mohamed Haji
7. Ali Ahmed Uki
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Zuhura Musa Lusonge2. Frederick Msigala
3. Amon Anastaz Mpanju4. Bure Zahran
5. Edith Aron Dosha6. Vincent Venance Mzena
7. Shida Salum Mohamed8. Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi.
9. Elias Msiba Masamaki10. Faustina Jonathan Urassa
11. Doroth Stephano Malelela12. John Josephat Ndumbaro
13. Ernest Njama Kimaya
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Haidar Hashim Madeweyya2. Alli Omar Makame
3. Adil Mohammed Ali4. Mwandawa Khamis Mohammed
5. Salim Abdalla Salim6. Salma Haji Saadat
7. Mwantatu Mbarak Khamis
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19)
TANZANIA BARA (13)
1. Honorata Chitanda2. Dr. Angelika Semike
3. Ezekiah Tom Oluoch4. Adelgunda Michael Mgaya
5. Dotto M. Biteko6. Mary Gaspar Makondo
7. Halfani Shabani Muhogo8. Yusufu Omari Singo
9. Joyce Mwasha10. Amina Mweta
11. Mbaraka Hussein Igangula12. Aina Shadrack Massawe
13. Lucas Charles Malunde
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Khamis Mwinyi Mohamed2. Jina Hassan Silima
3. Makame Launi Makame4. Asmahany Juma Ali
5. Mwatoum Khamis Othman6. Rihi Haji Ali
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. William Tate Olenasha2. Makeresia Pawa
3. Mabagda Gesura Mwataghu4. Doreen Maro
5. Magret Nyaga6. Hamis Mnondwa
7. Ester Milimba Juma
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Said Abdalla Bakari2. Mashavu Yahya
3. Zubeir Sufiani Mkanga
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10)
TANZANIA BARA (7)
1. Hawa A. Mchafu2. Rebecca Masato
3. Thomas Juma Minyaro4. Timtoza Bagambise
5. Tedy Malulu6. Rebecca Bugingo
7. Omary S. Husseni
TANZANIA ZANZIBAR (3)
1. Waziri Rajab2. Issa Ameir Suleiman
3. Mohamed Abdallah Ahmed
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (13)
1. Agatha Harun Senyagwa2. Veronica Sophu
3. Shaban Suleman Muyombo4. Catherine Gabriel Sisuti
5. Hamisi Hassani Dambaya6. Suzy Samson Laizer
7. Dr. Maselle Zingura Maziku8. Abdallah Mashausi
9. Hadijah Milawo Kondo10. Rehema Madusa
11. Reuben R. Matango12. Happy Suma
13. Zainab Bakari Dihenga
TANZANIA ZANZIBAR (7)
1. Saleh Moh’d Saleh2. Biubwa Yahya Othman
3. Khamis Mohammed Salum4. Khadija Nassor Abdi
5. Fatma Haji Khamis6. Asha Makungu Othman
7. Asya Filfil Thani
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20)
TANZANIA BARA (14)
1. Dr. Christina Mnzava2. Paulo Christian Makonda
3. Jesca Msambatavangu4. Julius Mtatiro
5. Katherin Saruni6. Abdallah Majura Bulembo
7. Hemedi Abdallah Panzi8. Dr. Zainab Amir Gama
9. Hassan Mohamed Wakasuvi10. Paulynus Raymond Mtendah
11. Almasi Athuman Maige12. Pamela Simon Massay
13. Kajubi Diocres Mukajangwa14. Kadari Singo
TANZANIA ZANZIBAR (6)
1. Yussuf Omar Chunda2. Fatma Mussa Juma
3. Prof. Abdul Sheriff4. Amina Abdulkadir Ali
5. Shaka Hamdu Shaka6. Rehema Said Shamte

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Februari, 2014

Leave your comment about Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba using the comment form below

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here