Vichekesho vya Kesi ya Mmasai na Mpare

0
10118
Masai na ngombe

Kulikuwa na wizi ulifanyika katika nyumba moja ya mpare pale hedaru na muhusika baada ya kufuatilia aligundua kuwa aliyemuibia ng’ombe wake alikuwa ni mmasai mmoja wa ng’ambo ya pili ya mto kikuletwa.

Mpare alimfungulia kesi ya wizi mmasai na mahojiano mahakamani yalikuwa kama ifuatavyo:

Mmasai; Wewe anasema mimi ameiba hiyo ng’ombe yako?

Mpare; Ndiyo

Mmasai; Aliingia kwa mlango ya nyuma ama ya mbele?

Mpare; Ya nyuma

Mmasai; Mekosa, aliingia kwa mlango ya mbele ya nyumba

Mmasai; Je, aliswaga ng’ombe dume akatangulia mbele au alikuwa nyuma?

Mpare; Dume alitangulia mbele

Mmasai; Mekosa tena, alibaki nyuma

Mmasai; Je ng’ombe alioibiwa iko ngapi?

Mpare; Ng’ombe  7

Mmasai; Amekosa kabisa, ng’ombe alikuwa 5 tu!!

Aha ha ha

Wewe hisi jaji alimhukumu au alimuachia huru huyo mmasai?

 

 

Acha maoni yako kuhusu kwa kutumia fomu hapa chini

Weka majibu hapa

Tafadhali weka maoni
Tafadhali weka majina yako hapa