Vichekesho kati ya mume na mke kanisani

7
22226
Familia na Maombi kanisani

Je unajua vichekesho kanisani? ulishasikia mojawapo, hebu fuatilia hii hapa.

Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar es salaam. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole.  Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia ibadani. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?

Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,

Mke:

“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”

Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada

Mume:

“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Kanisa  woote tuseme Amen”

HAKUNA ALIYESEMA AMEN badala yake baada ya kumaliza sala tu, alilishuhudia kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!

hii kali.

Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.

Leave your comment about Vichekesho kati ya mume na mke kanisani using the comment form below

7 COMMENTS

  1. Maoni:unajua waswahli wanasema fikir kabla kutenda ange2mia busara amwambie au amuamshe km mume asa amefanya hivo huon km heshima itashuka km mama ? je km huyo mume anahasira c anaachwa kisa mzahaa tena alimdanganya mume wakt wapo kanisani huon dhamb

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here